SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

27 August 2018

WANANCHI WARIDHISHWA NA UPATIKANAJI WA DAWA ZAHANATI YA NYAKABANGO - MULEBA

Bi Agnesi Mganga (kushoto) aliyefika katika Zahanati ya Nyakabango Muleba kupata matibabu ya mtoto akizungumza na Mwanahabari Dotto Mwaibale pichani kushoto, Bi Agnesi amesifia huduma za tiba zinazotolewa katika Zahanati hiyo kuwa ni za kulidhisha aidha ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Dkt.John Magufuli kwa kuimarisha sekta ya afya.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Nyakabonga Muleba kusini,Fausta Rugalinda,akiwa tayari kuzungumza na waandishi wa habari, kuhusu upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo ambayo amewapongeza (MSD) kwa kusimamia kwa ufanisi na gharama nafuu mfumo wa Kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba


 Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza,Cornelia G.Mwillawi pichani kulia akitolea jambo ufafanuzi kwa Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Nyakabango iliyopo Wilayani Muleba,Fausta Rugalinda wakati alipokuwa akikagua dawa zilizohifadhiwa kwenye stoo ya zahanati hiyo.
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Nyakabango wakati akiendelea kumuonesha Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza,Cornelia G.Mwillawiaina mbalimbali za dawa zinazopatikana katika Zahanati hoyo
Muonekano ndani ya Stoo ya dawa ya Zahanati ya Nyakabango
Bwana Mussa Pius mkazi wa Kata ya Nyakabango naye amesifia huduma za tiba zinazotolewa katika zahanati hiyo.
#Bukobawadau #Muleba26Agosti2o18

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU