SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

03 September 2018

HUDUMA ZA (MSD ) KYERWA ,KARAGWE,KAISHO

Wauguzi wa Zahanati ya Kaisho Wilayani Karagwe wakipokea maboksi yenye dawa kutoka MSD tayari kwa kuzihakiki kwa ajili ya matumizi kutoka kushoto pichani ni Yolanda Joseph,Editha Nyaruzi na Devotha Maganga
 Muonekano wa Jengo la Zahanati ya Kaisho iliyopo Wilayana Kyerwa
 Wauguzi wa Zahanati ya Kaisho iliyopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera,wakiendelea kuwajibika kubeba maboksi yenye dawa baada ya kupelekewa na Bohari ya Dawa (MSD) wilayani humo
Pichani kushoto Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD),Cornelia Mwillawi,akimuonesha fomu maalumu ya kujaza baada ya kukabidhiwa dawa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murongo, Dkt.Rashid Eid pichani kulia.
 Dr.Rashid Idd Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murongo Wiliyani Kyerwa akiongea na waandishi wa habari ambao walikuwepo mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Kagera zinazofanywa na Bohari ya Dawa (MSD)
 Pamoja na mambo mengine Dkt.Rashid Idd Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murongo alisema juu ya Changamoto kubwa waliyonayo ni wagonjwa wanaofika kupata huduma ya matibabu katika hiki kituo hicho kutojua lugha ya kiswahili hivyo ulazimika kutumia lugha ya alama kuweza kuelewana kwa mfano mgonjwa anaumwa kichwa basi atashika kichwa na kusema 'Omutwe au Mtwe na kama tumbo vilevile atashika tumbo"
 Dkt Rashid anaendelea kwa kwa kusema katika eneo hilo kunamuingiliano mkubwa wa watu kutokana na kuoleana kwani kuna Waganda waliooa Tanzania na Watanzania waliooa Uganda na kuwa kwa pande zote hizo mbili wananchi wake hawajui kuzungumza kiswahili zaidi ya makabila yao ya Kiganda,Kinyankole, Kihaya na Kinyambo,kwa ufupi historia ya Karagwe inafumua ukweli wa uhamiaji wa makabila mkoani Kagera.
 Bohari ya Dawa (MSD) Imeendelea kutoa huduma  kwa ufanisi mkubwa mkoani Kagera, mkoa wenye makabila makubwa mawili ambayo ni Wanyambo na Wahaya,Wanyambo huishi kwa wingi wilaya ya Kyerwa na Karagwe na Wahaya huishi kwa wingi wilaya ya Bukoba vijijini na Bukoba mjini na wananchi wote wanafurahia mpango huu wa kufikishiwa huduma kutoka MSD.
Sehemu ya Majengo Mapya ya kituo cha Afya Murongo kilichopo maeneo ya mpakani Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.
Majengo ya Upasuaji katika kituo cha Afya cha Murongo Wilayani Karagwe yakiwa yamekamilika.
Sehemu ya Stoo ya dawa katika kituo cha Afya cha Murongo
 Ndani ya Stoo ya dawa ya kituo cha Afya Murongo
 Mwanahabari Diana Deus  akiendelea kuwajibika.
 Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD),Cornelia Mwillawi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Denis Rugemalila ambaye ni tabibu wa Kituo cha Afya cha Murongo
 Mwanahabari Diana Deus akibadilishana mawazo na Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD),Cornelia Mwillawi pichani kulia
  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Dkt. Diocles Ngaiza, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upatikaji wa dawa kutoka Bohari ya Dawa (MSD).
Mfamasia wa Wilaya ya KyerwaDominic Malabeja katika picha na Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD),Cornelia Mwillawi
 Mzee Joshamu Mambo mkazi wa Kijiji cha Kyelele kata Nyakatuntu Wilaya ya Kyerwa akisungumza na wanahabari kuhusu upatikanaji wa Dawa kutoka MSD
Taswira nje ya majengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU