Bukobawadau

NDG JOANFAITH KATARAIA MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UVCCM TAIFA LEO AMEZINDUA KAMPENI YA KIJANI KATIKA KATA YA MSASANI JIJINI DAR ES SALAAM

Akizungumza na Vijana katika kongamano hilo la kijani lililofanyika katika uwanja wa Magunia amewataka Vijana hao kuendelea kufanya kazi kwa Ushirikiano ili kuendelea kusaidia kutatua Kero mbali mbali za Wanao waongoza bila kutegeana kila mmoja katika kipande chake.
Amesema “kiongozi anayemtegea kazi mwenzake asifikiri anamkomoa mbunge, mwakilishi, diwani , mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa bali anakihujumu chama cha mapinduzi.”
Alisema lengo la chama kuisimamia serikali ni kutaka kuendeleza msingi wa chama kuaminiwa na wananchi ili CCM iendelee kubaki madarakani kwa ridhaa kutokana na kuwajali pia kuwatumikia wananchi.
"Tunatakiwa kufanya kazi kwa nguvu moja ili kuendelea kuaminiwa na wananchi”.
"Alisema
 Aidha Ndg joan ameelezea juu ya kufurahishwa na kitendo cha Kuwakabidhi Bendera na Vifaa kazi mabalozi wa kata hiyo na kusema chama cha siasa ni kama mti ambao ikiwa shina litaimarika na kuwa madhubuti bila shaka matawi ya mti huo yatastawi na kunawiri wakati wote aidha ikiwa ni nyakati za kipupwe kiangazi au masika.
Pia ameendelea kusema midhali chama Cha Mapinduzi kipo katika mikono salama ya uongozi wa Mwenyekiti CCM Dk John Magufuli na Katibu Mkuu wake Dkt Bashiru Ally Kakurwa chama hicho kitazidi kuimarika kuanzia ngazi ya mashina hadi Taifa na kuendelea kushinda katika chaguzi mbali mbali.
Aidha Ndg Joanfaith ameupongeza uongozi wa Umoja wa Vijana wa Kata ya Msasani kwa kuendelea kuwaunganisha Vijana bila kujali makundi na kuwataka Vijana kote nchini Kuwa mabalozi wazuri wa chama kwa kuwa na maadili mema,uadilifu,uaminifu na kuheshimiana bila kujali rika.
*TukutaneKazini*
Katika picha ya pamoja
 Muendelezo wa matukio ya picha
 Aidha Ndg Joanfaith ameupongeza uongozi wa Umoja wa Vijana wa Kata ya Msasani kwa kuendelea kuwaunganisha Vijana bila kujali makundi na kuwataka Vijana kote nchini Kuwa mabalozi wazuri wa chama kwa kuwa na maadili mema,uadilifu,uaminifu na kuheshimiana bila kujali rika.
*TukutaneKazini*
Next Post Previous Post
Bukobawadau