JIJINI MWANZA MELI YA MV VICTORIA YANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO
Wafanyakazi wa Melini wakishirikiana na kikosi cha zima moto wakifanya jitihada za kuzima moto huo.
MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini(MSC)imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea sehemu mojawapo ya Meli hiyo.
Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zlizo patikana toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto ulipoangukia katika sehemu ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.
Wafanyakazi wa MSC wakitumia mashine maalumu ya kushushia mizigo ya kampuni hiyo wakitoa mabaki ya vitu vilivyounguzwa na moto.Picha zote kwa hisani ya GSENGO.
Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
Hata hivyo moto huo uliodumu kwa saa kadhaa ulifanikiwa kuzimwa ndipo juhudi za kuyatoa magodoro na mito yote ya makochi yaliyokuwemo ndani ya hifadhi ya mizigo ili kuhakiki uharibifu pamoja na kufanya tathimini kwa mali zilizo haribika.
Ndani ya masaa mawili moto huo ulikuwa umedhibitiwa na kikosi cha zima moto na uokoaji waliowasili katika eneo hilo muda mchache baada ya moto kuanza wakitumia gari lenye namba za ausajili STK 1965 Mali ya Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Ni hali halisi ndani ya Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
PICHA NA HABARI KWA HISANI KUBWA YA MDAU GSENGO.

Kwa upande wake afisa mfawidhi wa Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa
majini na nchi kavu(SUMATRA) kanda ya ziwa Josephat Loisimaye amesema
kuwa uzembe wa viongozi wa MSC ndio ambao ulisababisha kutokea kwa moto
huo.
Amesema kuwa viongozi wa MSC walipashwa kuchukua tahadhari mapema
kabla ya kuanza uchomeleaji katika sehemu ya Meli hiyo na kueleza kuwa
wanasubiri ripori ili waweze kuchukua hatua zaidi.
Hata hivyo Loismaye amesema kuwa Meli ya Mv Victoia iko salama na
itaendelea na safari zake kwenda Bukoba leo usiku kwa kuwa moto huo
haukuweza kuathiri mfumo wa injini ya Meli na kukipongeza kikosi cha
zimamoto kutokana na kufika mapema na kuzima moto huo vinginevyo Meli
hiyo ingeliteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa.