MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS AMPIGA RISASI MPENZI WAKE
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius,
anahojiwa na polisi kufuatia mauaji ya mpenzi wake nyumbani kwake mjini
Pretoria.
Kulingana na vyombo vya habari, mkuu wa polisi,
Sarah Mcira, aliambia wanahabari kuwa mwanamke aliyefariki nyumbani kwa
mwanariadha huyo alipigwa risasi kwenye mkono wake na kichwani.Hata hivyo hali iliyosababisha mauaji hayo bado haijulikani. Duru zinasema kuwa Pistorius huenda alimuua mwanamke huyo kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.
Pistorius alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki HII NI KUTOKA BBC