MASSAWE;Vijana Jishughulisheni na Ufugaji wa Nyuki ili kujikwamua kimaisha na Uchumi kuliko kutegemea serikali kuwatafutia ajira.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Fabian Massawe.
Muonekano wa Mzinga wa nyuki.
Mkuu wa mkoa wa Kagera ,Kanali mstaafu Fabiani Massawe ametoa wito huo katika uzinduzi wa kutundika Mizinga ya nyuki kanda ya ziwa uliofanyika katika wilaya ya Biharamulo hivi majuzi
Kanali Massawe alisema kuwa vijana ndio kundi kubwa lisilokuwa na ajira wala mapato katika mfumo wa maisha kwa wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 na wanahitaji kujiajiri kwa kutumia rasilimali na maliasili zilizoko katika mazingira yao.
Aliwataka vijana hao kujiunga kwenye vikundi vya pamoja na kuanzisha ufugaji wa nyuki na kuweza kupata asali na nta kisha kupata soko litakalosaidia kujiinua kiuchumi na kuongeza mapato katika familia ikiwa ni pamoja na kuepukana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwa kuvunja sheria.
Bw.Hatibu alisema takwimu inaonesha Tanzania ina hekta za misitu zipatazo Mil 34 ambazo ni makazi ya makundi ya nyuki yapatayo mil 9.2 yenye kuzalisha tani 130 za asali yenye thamani ya dola za kimarekani Bil.133 na kuinua kipato cha mwananchi.
Muonekano wa Mzinga wa nyuki.
Kundi
la vijana katika wilaya zilizoko mkoani Kagera
limetakiwa kujishughulisha na ufugaji wa nyuki kisha kujikwamua kimaisha kwa
kuongeza kipato ,kiuchumi kuliko kutegemea serikali kuwatafutia ajira.
Mkuu wa mkoa wa Kagera ,Kanali mstaafu Fabiani Massawe ametoa wito huo katika uzinduzi wa kutundika Mizinga ya nyuki kanda ya ziwa uliofanyika katika wilaya ya Biharamulo hivi majuzi
Kanali Massawe alisema kuwa vijana ndio kundi kubwa lisilokuwa na ajira wala mapato katika mfumo wa maisha kwa wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 na wanahitaji kujiajiri kwa kutumia rasilimali na maliasili zilizoko katika mazingira yao.
Aliwataka vijana hao kujiunga kwenye vikundi vya pamoja na kuanzisha ufugaji wa nyuki na kuweza kupata asali na nta kisha kupata soko litakalosaidia kujiinua kiuchumi na kuongeza mapato katika familia ikiwa ni pamoja na kuepukana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwa kuvunja sheria.
“Vikundi
vikiundwa na kuonesha uhai serikali itatoa ufadhili wa fedha na kuendeleza
miradi yenu kuliko kubaki maisha tegemezi na ombaomba kwa kutumia ardhi na
misitu hii ya asili jirani na hifadhi za Taifa”.Alisema Massawe.
Awali
Meneja na wakala wa huduma za Misitu kanda ya ziwa Bw. Haji Hatibu alisema lengo la uzinduzi wa utundikaji wa mizinga wilayani Biharamulo ni
kuhamasisha jamii kufuga nyuki kwa kutumia njia za kisasa na kuzalisha kwa
wingi zaohilo ambapo mizinga 100 yenye thamani ya Shilingi Milioni 7 , imezinduliwa na kutundikwa katika eneo la
misitu lililotengwa .
Bw.Hatibu alisema takwimu inaonesha Tanzania ina hekta za misitu zipatazo Mil 34 ambazo ni makazi ya makundi ya nyuki yapatayo mil 9.2 yenye kuzalisha tani 130 za asali yenye thamani ya dola za kimarekani Bil.133 na kuinua kipato cha mwananchi.
Kwa
mujibu wa Meneja huyo alidai kuwa kutokana na uvunaji jamii inaweza kutoa tani 9000 yenye thamani ya dola za kimarekani Bil
35 kwa kwa mwaka ambapo kwa sasa uwezo uliopo Tanzania inazalisha Tan 4800 za
asali yenye thanani Bilioni 4.9 na nta tani 324 zenye thamani ya Bil 648 sawa
na kutumia 3% ya uwezo tulionao wa
rasilimali zilizopo za asali na misitu .
“Kutokana
na ufugaji wa nyuki jamii inaweza
kujipatia gundi ya nyuki , sumu ya nyuki inayotumika katika tiba pamoja na
maziwa ya nyuki kama chakula na tiba “.Alisema hatibu.
Vilevile
alifafanua kuwa wananchi kwa kufuga
nyuki wataweza kupata huduma ya
uchavushaji wa mazao na kuongeza ubora wa mazao na kuanzisha biashara ya kuuza
makundi ya nyuki akiwemo malkia wa nyuki
kwa ajili ya kuongeza makundi yaliybora kwa kutumia fursa zilizopo.
Katika
hatua nyingine aliwaasa wananchi na wafugaji kujiepusha na uharibifu wa
mazingira kwa kuchoma na kukata miti na makazi ya nyukikwa kukosa maua na maji
kisha kuzalisha kiwango kidogo cha asali na nta na hata kuhama katika mizinga
baada ya kupata usumbufu wa makazi kimazingira.
Habari
na picha Na:Shaaban Ndyamukama.