Bukobawadau

MSANII WA FILAMU RECHO AFARIKI DUNIA

Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule ‘Recho’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam imethibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere.
Taarifa zinasema Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movie Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mshtuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. 

Tunatoa pole kwa familia na wasanii wote
Next Post Previous Post
Bukobawadau