Bukobawadau

MAPOKEZI YA MKUU WA MKOA MPYA NOV 14,2014

Mkuu mpya  wa Mkoa wa Kagera Bwana John Mongella aliyeteuliwa na  Rais Jakaya Kikwete Novemba 5, 2014 kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera amewasili rasmi mkoani hapa na kupokelewa na kukabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe.
Katika hafla fupi leo tarehe 14/11/2014 Kanali Mstaafu Fabiani Massawe alimsomea taarifa ya maendeleo ya mkoa Mhe. John Mongella na kumkabidhi taarifa hiyo pamoja na taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya serikali katika mkoa wa Kagera mwaka wa fedha 2014/15, na taarifa ya malengo ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2014/15
Kanali Massawe pamoja na kusoma na kukabidhi taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Kagera hakusita kuzitaja changamoto zinazoukabili mkoa kwa sasa ambazo ni Wahamiaji haramu hasa katika wilaya za Ngara, Kyerwa, Karagwe na Missenyi. Magendo ya mazao na hasa kahawa, nafaka, mazao ya misitu, bidhaa mbalimbali hufanyika kwenda nchi jirani.

Kilimo chetu kinakabiliwa na uzalishaji mdogo (tija); matumizi duni ya pembejeo na zana za kilimo; uhaba wa maafisa ugani na magonjwa hatari ya mimeaUfugaji nao bado ni wa kiasili wa ng’ombe aina ya ankole ambao uzalishaji wake wa nyama na maziwa ni duni;

Upungufu wa miundombinu ya mifugo kama majosho; magonjwa ya mifugo. Wavuvi wengi kutumia zana za asili kuvulia samaki. Michango ya halmashauri katika bajeti zake ni kati ya     2% hadi 4% ya bajeti nzima ya Halmashauri hizo.  Kwa hiyo hali ya utegemezi ni kubwa sana na hii inazipunguzia uwezo wa kuchangia katika maendeleo na utoaji wa huduma za kuridhisha.
  Mheshimiwa John Mongella Akipokelewa na Katibu Tawala Mkoa Bw. Nassor Mnambila na Kanali Mstaafu Massawe
 Akikiri kupokea ofisi na kuanza kuchapa kazi kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Kagera Mkuu wa mkoa Mheshimiwa John Mongella  alihaidi kuendeleza jitihada alizokuwa akizifanya Kanali Massawe katika kuwaletea wananchi  maendeleo kwa kushirikiana na watendaji walioko chini yake na wadau mbalimbali wa mkoa.
Pili, Mhe. Mongella alitoa angalizo kwa watendaji wa serikali kuhakikisha wanawahudumia wananchi katika ofisi zao bila kutumia milolongo mirefu ya sheria na taratibu. “Mwananchi hajui mambo ya standing order anachojali ni kupata huduma kwa wakati bila kucheleshwa, kwahiyo punguzeni milolongo mirefu ya utendaji wa kazi katika kutoa huduma.” Alisistiza Mhe. Mongella.
Tatu, Mkuu wa Mkoa Mongella alisistiza kuwa hapendi kufanya kazi kwa maneno mengi bali kwa vitendo na kuona , “Kama ni vyumba vya maabara nataka kuonyeshwa vyumba au kama ni zahanati nataka kuonyeshwa zahanati na siyo maneno maneno tu.”  Aliongeza Mkuu wa Mkoa Mongella.

Mwisho Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella alikemea na kutoa angalizo kuacha kutumia siasa au kuendekeza siasa katika maendeleo ya wananchi, alisema waache wanansiasa wafanye siasa zao lakini si katika kuwaletea wananchi maendeleo ambalo ndilo jukumu kuu la viongozi na watendaji wa serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha na anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa  tangu uhuru mwaka 1961.
 Mkuu Mpya wa Mkoa Bwana John Mongella akipokea Nyaraka na Kukabidhiwa Ofisi Rasmi na Mtangulizi wa Kanali Mstaafu Fabian Massawe.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akikabidhi Nyaraka zenye  taarifa ya Mkoa kwa Mkuu wa Mkoa mpya Mh. John Mpngella,anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bi Costancia Buhiye.
 Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi Costancia Buhiye, Mh. Massawe  kulia ni  Mkuu wa Mkoa mpya Mh. John Mongella
 Kwa pamoja wakitembea Kuelekea Mapokezi Uwanja wa Ndege wa Bukoba
Mheshimiwa John Mongella Akivishwa Skafu
 Katika utambulisho na Viongozi mbalimbali waliofika kumpokea.
Mh.Mkuu wa Mkoa akisalimiana na  Sheikh wa Mkoa wa Kagera  Sheikh Haruna Kichwabuta
 Mkuu wa Mkoa mpya Mh. John Mongella akisalimiana na Afisa Uvuvi Ndg Apolinary Kyojo
 Afisa mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Kagera Kapten Alex Katama akimkumbatia kwa furaha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mongella
 Sehemu ya Wadau waliofika kumpokea Mkuu wa Mkoa Mpya Mh.John Mongella
 Mkuu wa Mkoa Mh. John Mongella akitambua uwepo wa mwakilishi wa wanahabari Ndg Prudence Kibuka.
Burudani ya Ngoma maalum kwa ajili ya Mapokezi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mongella
 Mheshimiwa John Mongella akisaini Kitabu cha Wageni Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
NDIYO WALIYOJIRI WAKATI MKUU MPYA WA MKOA WA KAGERA AKABIDHIWA RASMI OFISI NA MTANGULIZI WAKE KANALI MSTAAFU FABIAN MASSAWE NOV 14,2014
 
Next Post Previous Post
Bukobawadau