Wema Sepetu amefunguka kuhusu Picha zake alizo post siku mbili
zilizopita akionekana ndani ya vazi la Harusi/ shela, Wema amedai kwamba
Picha hizo ni za Ndoa yake ya siri iliyofanyika hivi karibuni Bomani na
ndoa yake imefungwa ki serikali kwa sababu bwana harusi ambaye hakua
tayari kumtaja jina dini yake ni Mkristo wakati yeye Wema ni muislam na
ndoa hiyo ilihudhuriwa na idadi ya watu wasiozidi watano, na picha alizo
post kwenye mtandao zimepigwa katika hoteli ya Double Tree jijini dar
es salaam ambako kulifanyika hafla fupi.
Akizungumza na
Soudy Brown kupitia Uheard alisema kuwa aliamua kufunga ndoa ya siri
kwa kuogopa kupigwa ‘juju’ na mumewe kushindwa kumuoa.
"Mume wangu ni
Mtanzania na siyo maarufu na ndoa yangu ilihudhuliwa na ndugu zangu
wachache na ndugu wa mume wangu sikutaka watu wengi niliogopa kupigwa
juju na mume wangu asingenioa,"alisema Wema.
Alipoulizwa kuhusu
tatizo lake la kutoshika mimba mumewe alilichukuaje alisema kuwa hana
tatizo naye na amekubali kuishi hivyo hivyo.
Wema akaendelea kutoboa kuwa wanampango wa kusafiri hivi karibuni huenda
ikawa nje ya nchi kwa ajili Honey Moon, Wema ameolewa na mwanaume
mwenye umri wa kati si kijana si mzee na hajaolewa ndoa ya mitala, yeye
ndiye mke wa kwanza kwa mwanaume huyo
Chanzo: CloudsFM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comment:
Baraka nenda jami forum ukaone kuna picha za diector wa movie amayo wema ndio alivaa hizo nguo pichani movie na JB yeye akadai harusi sababu anaumi raha za Diamond
Nenda kasome director kasema hakun cha harusi na amekasirika sababu wema anasingizia kazi zake za filamu kuwa ni harusi...amewauzi na wamemsema instagram
KWA NINI HAMPENDEI MEMA WENZENU?KWANI YEYE KAMA AMESEMA AMEFUNGA NDOA WEWE KINACHOKUUMA NI NINI.HONGERA WEMA KALE HONEY MOON MDOGO WANGU
mwacheni ajinafasi kwani ni wakati wake WEMA kula bata na amupendaye na siyo kumsengenya kwa uamuzi wake alioufanya wa kufunga ndoa ya kiserikali ni mbmuzi yake.
ivi wa2 mnamatatzo gani mema yawe kwenu tu muacheni wema kama nyie hamumpend sie twampenda kama vp olewa we unaemponda nyoooooo
Post a Comment