MCHUANO WA UBUNGE MISSENYI KAZI KWA WAJUMBE
Leo tunakwenda kutazamia jimbo na wilaya maarufu kwa wasomi wengi nchii hii ambalo ni Nkenge na ni wilaya ya Missenyi ambapo tayari wameomba tume ikubali jimbo na wilaya viwe na jina moja ambalo ni Missenyi
Mchuano unasadikika kuwa mkali mwaka huu ndani ya chama cha mapinduzi kuliko kwenye chaguzi za jumla kutokana na historia za siasa za Missenyi kuwa za upande mmoja katika tafiti leo tunapitia baadhi ya watu wenye nguvu na wanaotajwa katika vijiji na vitongoji mbalimbali .
1. Frolent Kyombo huyu ni mbunge aliyeko madarakani akionekana kuwa bado na wafuasi kwa miradi na mafanikio makubwa ya Serikali ya hawamu ya sita anatarajiwa kutoa upunzani mkali huku maeneo mengine kama ubunifu na kuunganisha wanamissenyi vikitajwa kuwa kama ndio kushindwa kwake maana mpaka sasa jimbo limekuwa na migogoro mingi huku viongozi wengi wa chama hawako upande wa mbunge kwa kuwa alishiriki kampeini za ndani ya chama na kwa bahati mbaya watu aliwaunga mkono hawakupita na kumekuwa na minunguniko mikubwa
2. Assumpiter Mshana huyu aliwahi kuwa mbunge 2010_2015 lakini bado ameendelea kuamini kuwa wanaccm wanaweza kumpa nafasi ya kuongoza tena kwaiyo analo kundi na 2020 alikuwa mshindani wa karibu wa mbunge aliyeko sasa madarakani wengi wanavutiwa na siasa zake za Umasikini siyo fungu letu ,Alama kubwa ni Mfumo mzuri alioweka wa kuwasaidia kina Mama kupitia SACOSS
3. Evance Kamenge huyu ni kijana mdogo mjasiliamali na mchumi ambae anatambulika kama public figure ni mjenga hoja mzuri kwenye vyombo vya habari na midaharo mikubwa nchini amekuwa kijana wa mfano kwenye mambo mengi yeye ni mkulima na mfugaji mzuri ila ni mkurugenzi wa makampuni anamiliki KGM (Kamenge gold mine geita) Vijana na watu wengi wanavutiwa na hoja zake hasa za kuwainua watu kiuchumi na misimamo yake ya kutaka viongozi kuwajibika sawa sawa ni msomi mzuri na anayefanya mambo kwa jamii yake mda sasa na mwaka 2020 alikuwa kati ya washindani watatu wa karibu wa mbunge wa sasa
4. Projetus Tegamaisho huyu ni mwenyekiti wa halimashauri na diwani wa kata ya kyaka ambae hivi karibuni ameonekana kukubalika sana katika jimbo huku akionesha uwezo mkubwa kwenye kusimamia miradi ya halimashauri ana wavutia wengi kwa kuwa anaishi wilayani hapo na anashiriki mambo ya kijamii sana changamoto yake ni Ukanda na historia ya Siasa Ya Missenyi inayoamliwa na Tarafa ya Kuziba Ni Mara Chache Mtu kutoka Tarafa ya Misseny kiuhalisia kuwaongoza wasomi hawa.Ingawajee Ukweli ni Kwamba toka Kifo cha Mzee Katunzi huyo Jamaaa Tegamaisho ndiye ameshikilia Siasa za Missenyi japo zipo tetesi kuwa Si Mtu wa Ukanda huo maana yeye ni mzaliwa wa Bukoba vijijini licha ya kuamia Missenyi na kuweka Mizizi mpaka kukubalika na Kuaminiwa
Yote Juu ya Yote kazi kwa wajumbe
5. Kundi hili Wanaitwa Matection ni Wale Watia Nia Wajanja wajanja wanaotumia kivuri cha Siasa kuwalaghai Watu na kujipatia upenyo wa kuficha Maovu yao Inasemekana upenda kujipa nafasi kama Maafisa sehemu flani nyeti hama Usema wametumwa kwa Kazi Maalum ,Ndo wale uwezi kupata Kisa chochote kinachoweza kuzungumizia mhusika alitenda wema wakati flani au Sehemu flani zaidi ya Kuwanunulia Watu Pombe na Kujikweza Yetu Macho
6 .Hawavumi Lakini Wanatikisa Hili ni Kundi la Watu flani Makini wanaojua dhamani na wajibu wao Kwenye Jamii hapa Utajikia Majina Kama Thobias ,Julias Na Mzee wa Mutukula wakitanjwa tanja Siasa za Missenyi
Kwa leo nimewaletea jimbo la Missenyi jimbo ambalo ni lango la nchi yetu kuelekea kwa majirani zetu
Na Mwandishi wetu habari za utafiti
#LiwaloNaLiwe