SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

23 November 2013

MANENO YA MWIGULU NCHEMBA BAADA YA ZITTO NA DR KITILA KUVULIO VYEO; "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA"

Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu. Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa. Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo kwenye list. I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni. Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi. Haya ndio madhara ya AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA, HOFU NDIO HUTAWALA

5 comment:

Anonymous said...

Nchemba acha unafiki leo ndio unajifanya kumkubali Zito wakati siku zote unampinga, tunaelewa kuwa umeumia sana baada ya kuona watu mliokuwa mnawatumia wamewekwa pembeni, siku zote ukae ukitambua kuwa hiyo ndio Chadema

Anonymous said...

Chadema juuuuuuuuu+100000000000

Anonymous said...

nyie watangulizi hapo juu suala hapa sio zito wala nani sisi wanachadema tunataka hizo tuhuma zijibiwe basi tujue mbivu na mbichi sasa katiba kuvulugwa au ruzuku kutumiwa na baba mkwe na mkwe ndio kosa la mtu kufukuzwa au kuuwa kama walivyo tangulia tupe majibu watz tuna akili kila kijana wa nchi mpenda siasa rol model wake ni zito awe chadema au ccm au cuf huo ndio ukweli.

Anonymous said...

kwan chadema humjui kwama ni taasisi ya mbowe and mtei family Silaa ni chambo tu naye cku zinesabika tuu kama ulikuwa kwenye mkutano wa chadema pale ubungo plaza wa chama utaelewa nini namaanisha chama kizuri sana ila kuna makapi wengi sana na ndio viongozi kama alivyokuwa sumaye wazir mkuu kwanza uongozi then ndio usomee baada ya kustaafu does not make sence.

Anonymous said...

We nchemba ondoa uchuro hapa mnafiki mkubwa wewe.

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU