Rais
wa Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo
katika viwanja vya Karimjee kufuatia
kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021 jijini Dar es Salaam
Rais
wa Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kilichotokea tarehe 17 Machi 2021 jijini Dar es SalaamMakamu
wa Rais, Mstaafu Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo
katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli .
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma akisaini kitabu cha maombolezo katika
viwanja vya Karimjee
kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati
John Pombe Joseph Magufuli .
Spika
wa Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mhe. Zubeir Ali
Maulid akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo
cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe
Joseph MagufuliBalozi
wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Ali Abdulla – Al Mahrouq akisaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli .Balozi
wa Somalia nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Hassan Abdi akisaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Balozi
wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa akisaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Balozi
wa Sudan nchini Tanzania, Mhe. Jaafer Nasir Abdalla akisaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ...
Naibu
Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberte Cocconi akisaini kitabu cha maombolezo katika
viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Na mwandishi wetu
Marais
wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi waandamizi wa Serikali na
mabalozi waonaziwakilisha nchi zao hapa Nchini wamewataka watanzania kuendelea
kudumisha uzalendo, fikra na maono aliyokuwa nayo Hayati Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli ili kuiwezesha Tanzania kukua kimaendeleo
Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe.
Jakaya Kikwete amesema kifo cha Hayati Magufuli hakikutarajiwa hasa wakati huu
ambapo taifa
lilimuhitaji
na kuwasihi watanzania kudumisha mema aliyoyaasisi kwa maslahi ya taifa.
“Kwa
kweli kifo chake hakikutarajiwa, tulitegemea kwa kweli aendelee kuliongoza
taifa kwani katika mhula wake wa kwanza aliliongoza taifa vizuri sana…….naamini
kuwa yale ambayo hayakukamilika, Rais wa Jamhuri ya Tanzania mhe. Samia Suluhu
Hassan atayaendeleza kikamilifu,” Amesema Dkt. Kikwete na kuwasihi watanzania
kuendelea kudumisha uzalendo, fikra na maono aliyokuwa nayo Hayati Dkt.
Magufuli.
Rais wa Awamu ya Pili, Mhe. Alhaji Ali Hassan
Mwinyi nae amefika katika viwanja vya Karimjee na kusaini kitabu cha maombolezo
akifuatiwa na Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano
wa Tanzania Mhe. Mohamed Gahib Bilali, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim
Juma na pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai nae pia amefika na
kusaini kitabu hicho akifuatiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar mhe. Zubeir Ali Maulid ambaye amesema kuwa Hayati
Magufuli katika kipindi kifupi cha uongozi wake amefanya mambo mengi
yatakayosalia kuwa historia katika taifa la Tanzania.
“Msiba huu ni wetu sote watanzania na umetugusa
sana kwani hayati Magufuli ameyafanya
mengi katika mhula wake wa
kwanza
ambapo mengi hayo tumekuwa tukinufaika nayo sisi watanzania…..kwa sasa
tushikamane kudumisha umoja wetu ili kuweza kusonga mbele kimaendeleo,” Amesema
Mhe. Maulid
Aidha,
mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini nao wameungana na watanzania
kuomboleza kifo cha Hayati Dkt. Magufuli kwa kusaini kitabu cha maombolezo
ambapo baadhi yao wamemuelezea kuwa katika uhai wake Hayati Magufuli alitamani
kuiona Tanzania inayojitegemea kiuchumi na watu wake kuondokana na umasikini.
Naibu Balozi wa Burundi nchini Tanzania, Mhe.
Prefere Ndayishimiye amesema kuwa msiba wa Hayati Magufuli umewagusa sana kwani
alikuwa
kiongozi
aliyependwa na kujulikana na bara lote la Afrika.
“Amefanya
maendeleo makubwa ambapo naamini kuwa vizazi vijavyo vitayaona na kuendeleza
pale alipoishia Dkt. Magufuli,” Amesema Naibu Balozi
Kadhalika,
mbali na viongozi wastaafu pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali wananchi
wa kada mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kusaini kitabu cha maombolezo na
kumuelezea hayati Magufuli kuwa alikuwa kiongozi aliyeweka maslahi ya nchi
mbele kwa manufaa ya watanzania.