Bukobawadau

MKURUGENZI WA MANISPAA AWAITA WANANCHI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia, amewataka wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
Wito huu ulitolewa leo, Septemba 25, 2024, wakati zoezi rasmi la uboreshaji likianza katika Mkoa wa Singida, hususan Jimbo la Singida Mjini.

“Nawakaribisha wananchi wote wa Manispaa ya Singida katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Vituo vinapatikana katika kata 18 zote, kwa wale wenye sifa za kujiandikisha na wale wanaoboresha na kuhamisha taarifa zao,” alisema Bi. Kataraia.

Zoezi hili linatarajiwa kudumu kwa siku saba, likitarajiwa kukamilika Oktoba Mosi, 2024.
 Mkurugenzi huyo alisisitiza umuhimu wa kujitokeza kwa wingi ili wananchi waweze kuchagua viongozi wao bora ifikapo 2025.
 kama Rais, Wabunge, na Madiwani mwaka 2025,” aliongeza.

"Tume Huru ya Uchaguzi  wamejipanga vizuri naona vifaa vipo vya kutosha na watoa huduma  wapo katika vituo"
 


 

Next Post Previous Post
Bukobawadau