Bukobawadau

MAFURIKO YALIYOUKWAZA MJI WA BUKOBA JANA SASA YAPUNGUA NA KURUHUSU WANANCHI KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU

Mafuriko katika mji wa Bukoba yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha kwa muda mrefu Mei 26, 2019 sasa yapungua na maji kuondoka katika makazi ya watu ambapo wananchi nao wameanza kurejea katika makazi yao na baadhi ya barabara zilizokuwa zimefungwa kutokana na maji kujaa sasa zimefunguka na zinafanya kazi na kuruhusu shghuli za kawaida kuendelea.
Na: Sylvester Raphael 
Akitoa taarifa ya tathimini ya awali juu ya mariko hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti Mei 27, 2019 alisema kuwa kwasasa hali imeanza kuwa sawa na wananchi sasa wameanza kurejea katika makazi yao baada ya maji kupungua kwa asilimia 85% katika makazi ya watu.
Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa mvua iliyonyesha Mei 26, 2019 kuanzia saa 3:00 asubuhi na kusababisha mafuriko katika mji wa Bukoba yalisababisha kifo cha mtoto mmoja wa miaka 10 aliyetoka nje wakati wa mvua kwenda kujisaidia na kukumbwa na maji yaliyopelekea kifo chake.
Kutoakana na mafuriko hayo nyumba moja ilianguka katika maeneo ya Kagondo, nyumba 32 ziliathirika na mafuriko, karavati moja omukigusha liliharibiwa, nguzo moja ya umeme na bomba la maji moja vilipata madhara, pia baadhi ya makaravati yaliziba kutokana na wingi wa maji na kuambatana na taka nyingi.
 Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa baadhi ya madaraja yaliyokuwa yamefurika maji na kufanya barabara kutopitika sasa madaraja hayo yanapitika kutokana na maji kupungua kwa kiasi kikubwa, aidha Serikali inaendelea kushirikiana na wananchi kuzibua mitaro na kutoa elimu ili wananchi waendelee kuchukua tahadhari kuwadhibiti watoto kutotoka nje wakati wa mvua kwani mvua zinaendelea kunyesha. yaliambatana na uchafu mwingi unaoweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Akielzea chanzo cha mafuriko hayo Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa ni baadhi ya wananchi kuendesha shughuli za kibinadamu kandokando ya mto Kanoni na kubana kingo zake kusababisha maji kupasua kingi hizo na kufurika katika makazi ya watu. Pia alisema kuwa tatizo hilo Serikali italifanyia kazi mara baada ya hali kutengamaa kabisa na wananchi kurejea kwa asilimaia 100% kwenye makazi yao.

Wito wa Mkuu wa Mkoa Gaguti ni wananchi kuchukua tahadhari za kiafya kwani maji yaliyofurika katika makazi yao yaliambatana na taka nyingi ambazo zinaweza kusababisha magojwa ya mlipuko kama kipindupindu au kuhara na kuhara damu.
Barabara ya Uganda Maeneo ya Linas Club
Mwisho


Next Post Previous Post
Bukobawadau