Bukobawadau

Kushuka daraja kwa Birmingham City ndio chanzo cha kufuta safari ya Tanzania

Birmingham City wameamua kufuta safari yao ya kwenda Tanzania.
City, ambao wameshuka daraja katika ligi kuu ya England msimu huu walikuwa wasafiri kuja Tanzania kupambana na Simba na Yanga katika mechi za kirafiki.
Baadhi ya sehemu za jengo la club ya Birmingham City.

Hata hivyo watayarishaji walishindwa kuthibitisha utaratibu wa safari hiyo katika muda waliopewa.Bukobawadau bado unajiuliza ni kwa nini viongozi wa timu za Simba na Yanga awajaweka bayana swala hili.
Kama ilivyo kuwa mwanzo kwa mwenyekiti wa Simba Ismail Adden Rage alivyolisemea kwa mbwembwe kwenye vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

Mabingwa hao wa kombe la Carling sasa wanatafuta nchi ya kwenda kucheza mechi za za kalba ya kuanza kwa msimu
.
Next Post Previous Post
Bukobawadau