Bukobawadau

Liverool yaifanyia 'mauaji' Fulham.

Liverpool imejiongezea matumaini ya kumaliza katika timu nne za juu baada ya kuiangushia kisago cha mabao 5-2 Fulham kwenye uwanja wa Craven Cottage.
Rodriguez amefunga magoli sita katika mechi mbili

Maxi Rodriguez alifunga mabao matatu peke yake, huku akifunga goli la kwanza katika sekunde ya 32.

Maxi alifunga goli la pili katika dakika ya saba, na lake la tatu katika dakika ya 70. Dirk Kuyt na Luis Suarez walifunga magoli mengine ya Liverpool.

Moussa Dembele na Steve Sidwell walifunga magoli mawili ya Fulham, ambao walikuwa wakicheza nyumbani.
Next Post Previous Post
Bukobawadau