Bukobawadau

WAJUMBE WA GADDAFI WAZUNGUMZA NA URUSI:Gaddafi aahidi kupambana mpaka mwisho.

Kanali Gaddafi aahidi kupambana hadi mwisho

Wajumbe wa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi wanatarajiwa kufanya mazungumzo na maafisa wa Urusi mjini Moscow.

Urusi ilisema, mazungumzo tofauti ndani ya Moscow na waasi yalitarajiwa kufanyika, lakini yakafutwa kutokana na "sababu za kiufundi".

Bunge la nchi hiyo Kremlin limekataa kuwakubali waasi kama viongozi halali, na bado wana uhusiano mzuri na Kanali Gaddafi.

Siku ya Jumatatu, mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ameshikilia kutolewe hati ya kukamatwa kwa Kanali Gaddafi.

Mwendesha mashtaka huyo Luis Moreno-Ocampo alisema, mtoto wake wa kiume Seif al-Islam, na mkuu wa idara ya ujasusi Abdullah al-Sanusi wamehusika kwa "mashambulio yaliyopangwa kwa ufanisi na kutapakaa" kwa raia.

Majaji wa ICC bado wanatakiwa kuamua iwapo watoe hati ya kukamatwa kwao au la.

Serikali ya Libya tayari imesema itapuuza hatua hiyo.

Katika tukio tofauti, milipuko ilisikika karibu na makazi ya Kanali Gaddafi mjini Tripoli mapema siku ya Jumanne.

Maafisa wa Libya baadae waliwachukua waandishi wa habari kwenye eneo hilo na kuwaonyesha majengo, yaliyokuwa yakiwaka moto baada ya kushambuliwa kwa kilichoonekana kufanywa na majeshi ya anga ya Nato.

Msemaji wa serikali alisema miongoni mwa majengo hayo ni ofisi ya jeshi la usalama.
Next Post Previous Post
Bukobawadau