Bukobawadau

Senene Asubuhi ya leo na kila mdau anaambiwa kama wewe ni mzaliwa wa Kagera.... ( Taliwo Atakaibaga Nsenene)

Nje ya soko kuu mjini Bukoba,anaonekana Ndg Hamza muuza senene maarufu saana akiwa na senene walio tayari kwa kitoweo

Senene ni kitoweo asa mkoani Kagera.Zipo aina nyingi za wadudu ambao katika baadhi ya makabila hapa nchini hutumiwa kama kitoweo na pia katika uzalishaji wa bidhaa za vyakula kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Lakini senene ambao hupatikana kwa wingi mwishoni mwa kila mwaka,japo kutokana na mabadiriko ya kimazingira kwa sasa senene awana msimu maharumu..wanaweza kutoka kila baada ya miezi mitatu.Senene ni miongoni mwa wadudu wanaotumiwa zaidi na kabila la Wahaya mkoani Kagera kama kitoweo, pengine kuliko kabila jingine unalolifahamu.

Ili kufanywa kitoweo,wadudu hawa jamii ya panzi au nzige hukamatwa, kuondolewa mbawa, miguu, papasi na mikia yake kisha kukaangwa kwa mafuta au hata bila mafuta. Katika hatua hii huwa tayari kwa kuliwa na chakula chochote ambacho huwa kimeandaliwa.

Lakini si wakati wote senene hawa huandaliwa kwa njia hii, kwani wakati mwingine wingi wao husababisha wale wanaowakamata kushindwa kuwatengeneza. Inapofikia hatua hii senene hawa huchemshwa katika maji kwenye sufuria kubwa na baada ya muda huondolewa na kukaushwa kwa kuwekwa kwenye chanja juu ya moto. Chanja hii inajulika kwa jina la kihaya 'olushero'.

Daaaahh!!ndivyo anavyo onekana Mshikaji aking'aka baada ya mtoza ushuru wa manispaa ya bukoba kumfikia nakumtaka atekeleze malipo ya ushuru.
Machalii wao uwokota senene wanao rukaruka na kuwapiga bei.unaambiwa mjini mipango

Mara nyingi senene wanaokaushwa, huifadhiwa kwa lengo ya kutumika kama kitoweo kwa familia husika na zaidi hutumwa kama zawadi ya heshima kwa wapendwa wa familia hizo, hasa wanaoishi mbali ambako si rahisi kupatikana
.
Gharama sio kuwanunua Senene au kuwapa?....gharama kubwa ni kuwatengeneza ,kuwamenya, kuwaandaa kama hivi unavyo jionea.
Next Post Previous Post
Bukobawadau