Bukobawadau

KUMBUKUMBU juu ya sakata la Umeme Nchini,Ikiwa leo ni Siku ya BAJETI ya Wizara ya Nishati na Madini-Mama Kilango awashamoto Bungeni!!!!

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja
Anne Kilango Malcela

RAIS Jakaya Kikwete aliingilia kati mvutano uliokuwepo kati ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhusu upitishwaji wa nyaya za umeme wa kilovolti 132.

Habari za uhakika zilisema kuwa Rais Kikwete aliagiza Wizara ya Nishati na Madini kuandaa kikao kitakachowakutanisha wadau mbalimbali ili kutatua tatizo hilo.

Hatua ya Rais Kikwete kuingilia kati suala hilo ilikuja baada ya juhudi za kikao cha awali kati ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Zachary Kakobe kutofikia makubaliano.


Mchungaji Kakobe akilalamika juu ya kupitisha nguzo za umeme kwenye kanisa lake.Akiwa na Waumini waliamua kupiga kambi saa 24 katika eneo la kanisa hilo, huku wakiwa wamevalia fulana maalum zilizoandikwa kwa mbele ‘TANESCO Muogopeni Mungu’ na nyuma ‘Baada ya Richmond Mmegeukia Kanisa’.
Hivi punde Mama Anne Kilango Malcela akichangia bajeti ya wizara ya nishati na madini bungeni amesema:Hakuna jema lolote katika vita isipo kuwa mwisho wake ivyo serikali isiogope kufeli kabla aijaingia kwenye mtihani.

Mama Kilango akionyesha hisia kali na uchungu amesema awezi kuhunga mkono bajeti mpaka waziri Ngeleja atowe maelezo yanayokidhi,Pia ameiomba Serikali ikamate kitu kimoja kuliko kupapasa papasa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau