Bukobawadau

Muhimu kuhusu sudan ya kusini ikiwa leo ni siku ya UHURU..Imeandaliwa na Mc

Idadi ya watu: 7.5-9.7 milioni
Ukubwa: 619,745 kilometa za mraba (239,285 maili), kubwa kuliko Uhispania na Ureno zikijumuishwa pamoja.
Lugha kuu: Kiingereza, Kiarabu (zote ni rasmi), Kiarabu cha Kijuba, Kidinka
Dini: Za kijadi/asili, Wakristo kidogo
Biashara ya nje: Mafuta
Moja ya nchi maskini kabisa duniani: Idadi kubwa ya vifo vya akina mama wajawazito; watoto chini ya miaka 13 hawasomi; 84% ya wanawake hawajui kusoma na kuandika.
Uhusiano na Sudan: Kugawana madeni na mafuta ; migogoro ya mipaka; uraia
Usalama: Takriban vikundi saba vya waasi.


CHANGAMOTO NYINGINEZO MBELENI
Wakati huohuo, Marekani imeitaka serikali ya Bw Bashir kuyaruhusu majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani kuendelea kubakia kaskazini, kufuatia vitisho kutoka Khartoum kuyafukuza kutoka majimbo ya Kaskazini ya Kordofan Kusini na Blue Nile.

"Ni muhimu kwa Umoja wa Mataifa kuruhusiwa kulinda amani kikamilifu katika maeneo hayo kwa kipindi kirefu zaidi," alisema Susan Rice, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Mwandishi BBC anasema kuifanya Sudan ya Waislam Kaskazini na Kusini kuwa tulivu kwa muda mrefu baada ya sherehe kuisha itakuwa ni changamoto kubwa.

Pande zote mbili lazima zikamue juu mambo kama kuweka mpaka mpya na namna ya kugawana madeni na utajiri wa mafuta.

Wachambuzi wanasema kipaumbele kwa Khartoum kitakuwa kufanya mazungumzo juu ya mkataba mzuri wa mapato ya mafuta kwa sababu visima vingi viko Kusini.

Kwa sasa, mapato hayo yanagawanwa sawa kila upande.
Khartoum ina nguvu kwa sababu mabomba mengi ya mafuta yanaelekea Kaskazini kwenye bandari ya Port Sudan iliyoko bahari ya Sham

Kipande ninacho hisi mie Mc kitaleta shida ni URAIA
Uraia pia ni suala ambalo bado halijafanyiwa maamuzi.
Kwa mujibu wa redio ya Taifa Sudan, uraia wa Wasudan Kusini wanaoishi kaskazini umekwishafutwa.

Mapema wiki hii, maelfu ya wafanyakazi Wasudani Kusini wanaofanya kazi kaskazini walilazamika kuacha kazi zao kabla ya kugawanyika.

Next Post Previous Post
Bukobawadau