Bukobawadau

MATUKIO YA SHEREHE ZA KUWAPOKEA MA-HAJI NA MAHAJATI WA VIJIJI VYA:RUHOKO NA NGARAMA -KATORO PIA NA BUKOBA MJINI

SHEIKH HARUNA KICHWABUTA
Unapokuwa kiongozi wa watu ni razima uwe mtunishi wao.Kauli hii imethibitishwa na sheikh Haruna kichwabutta,sheikh wa manispaa ya bukoba na sheikh wa wilaya ya bukoba vijijini pale ilipomrazimu jana kuhudhuria zaidi ya sherehe tatu za mapokezi ya ma haji na mahajati zilizokuwa katoro umbali wa zaidi ya kilomita 160 kwenda na kurudi kwa kutokea Bukoba Mjini

Kama anavyoonekana katika picha sheikh aliwaasa sana waisilamu wa kijiji cha ruhoko kutimiza nguzo hii ya tano kwa wenye uwezo kwani mwenyezimungu s,w hana dhamana na muislamu yoyote anayekufa bila kutimiza nguzo hii ya tano ya uisilamu hali ya kuwa ana uwezo aidha aliongeza kwa kusema mtu yoyote anayejidanganya kuchelewa kwenda hija ati kwa kusubiri kumiliki magari ya kifahari na majumba ya kifahari,mtu huyo kama atakufa kabla ya kwenda hijja basi mtume mohammaad s,a w anasema mtu huyo anakufa akiwa myahudi au mnaswara.

Waislam wa Ruhoko wakisikiliza waadhi wa Sheikh Haruna
Hajati Hafswa(afisa)mke wa haji Yahaya katakweba akiwa nyumbani kwake Ruhoko
Bukobawadau blogspot tunampa Ongera Hajati Afisa.
Walio wengi hudhani kuwa sheikh Ismail ni mtoto wa Alhaji SheliSheli, picha hii ya pamoja kati yao inaondoa wasiwasi huo kwa walio wengi kufananisha.Shukurani za dhati zimwendee hajati Hafsa aliyewakutanisha.
Wahida,Ummusalma na Ummulkheri
Pichani Hajati Hafswa akiwa na familia yake
Hajati Mastura Zarwano
Haji Mohammadi Sewagudde kulia akiwa na Sheikh Magundusi kutoka Masaka Uganda
Sheikh Haruna Kichwabuta akisikiliza waadhi kutoka kwa sheikh Magundusi.
Hatimaye Ziara Ya kuwatembelea mahaji na mahajati iliishia Bukoba mjini kwa haji Rashird Banyankasaba Tororo pichani na mkewe bi Ashura Habibu Almasi
Pichani sheikh Ismail anaonekana akimsisitizia jambo rafiki yake Haji Rashird B.Tororo.
Bukobawadau tunawapa pongezi Mahajati wote na Ma-Haji kwa kutimiza nguzo kuu ya tano ya dini ya kiisilam!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau