Bukobawadau

HII LEO HEKA HEKA ZA X MASS;Foleni Bank na hali ya mvua usipimee!!,Soko la Senene Kwishine!!!,Wageni ni Wengi japo Mbwembwe Si Kivileeeee!!!!!!!

Camera yetu imeangaza maeneo ya sokoni jioni hii,kikubwa ni ile hali tuliyo izoea ya soko la senene ,kwa siku ya leo ni tofauti kwani eneo lote senene walibaki kwa mdau mmoja tu hii yote ni kutokana na wingi wa wageni juu ya siku kuu ya krismas.
Bukobawadau hii tumeipenda

Siwezi kusema huyu mama ndie mteja wa mwisho kwa leo bali kwa mhuzaji ni kama vile anamwona mteja wa lala salama.
Kiwanja Cheupeeeeeeeeeee!!!!!sasa ni maegesho ya magari kama unavyo jionea mdau kwa lugha nyingine tunaweza kusema Senene kwishineeeeee!!!!
Libeneke stend ya Bugabo wao wapo kijijini ila chakula siku zote utoka mjini...
Kulikoni wadau pande za Bugambo?!!!kama unavyo jionea gari hili Canter likiwa limepakia mizigo mbalimbali hata mkungu wa Ndizi ni safari ya kuelekea Bugabo

Ni Saa moja kasoro ya jioni hii,nakutana na wadao katika hali hii Bank ya CRDB iliopo barabara ya Kashozi
Kwa haraka haraka unaweza kuwaza kwamba watu ni watumiaji ila Bukobawadau katika hili tunaweza kusema hali ya uchumi sio nzuri kabisa
Bi Eunice Ruhangisa akisalimiana na Mzee wake yumo ndani ya Gari na wa nyuma aliye simama ni kaka yake.kama walivyo kutwa katika pita pita zangu jioni hii
Jengo jipya la Karamage zamani ilikua kwa Mistry.
Kwambali namwona bwana kaka akielekea ndani ya Sadath Boutique na hapo nazidi kuamini kwamba biashara ni matangazo.
Bubokawadau tunatoa Shavu kwa mdau wetu Sadath Boutique
Duka hili lipo barabara ya zamani ya soko kuu mjini hapa
Mkabala na Soko kuu
.
Nikielekea Home Buganguzi hili ni Daraja la Kyabakoba.
Picha hii rukhsa kushare wadau.
Kushoto ni mdau Salum Mawingu(organizer),katikati ni Haruna Goronga na mwisho ni Majid Kichwabuta.
Hapo namkumbuka Marehemu Muhazi ukanda huu kwa kukienzi chama cha ushirika cha Mbatama
Hapo Masikani kwa Galiatano nyumbani Buganguzi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau