Bukobawadau

KIROYERA TOURS KATIKA LIBENEKE LA MIAKA 50 YA UHURU :Watuma salam kwa Bukobawadau na Wadau wote kiujumla nasi tunasema tupo pamoja na wao!!!!!

Ndugu yangu MC na wadau wa Bukoba blog!!

Ukweli kijana wetu MC unakuja kuwa tajiri wa information very soon kwani blog yako ya Bukoba wadau inapendwa sana- keep it up watu wanasema hawaoni haja ya kuja Bukoba vile wanapata daily events kupitia blog ya BKB Wadau. Najua mwanzao mgumu lazima kuwe na watu wenye mawazo tofauti lakini moja na moja ni mbili.


Nikaulizwa maswali M.C ni mwanahabari- nikawaambia soma profile ya kijana ni mjasiriamari sio mwandishi wa habari na ndiyo maana achelewi kuwapasha- Kiutalii umenikwaza kwamba watu wanaona kila kitu hivyo hawatakuja Bukoba .

Group ya pili ikasema tunavutiwa inabidi tuje bka tuone macho kwa macho hapo nikafurahi na kuwaambia kuwa Said kaloli atakuwa akitumbuiza December 25 na BK Sunday Kaitaba- nitakutumia picha na tangazo uliweke na kulisemea tutaelewana tu

Swala la muhimu- Katika kusherekea miaka 50 ya uhuru Mkoa wa kagera uliteua baadhi wa wajasiriamali kuwakilisha wadau wengine katika maazimisho hayo hapa Dar es salaam- . Niliona kwenye taharifa ya Habari TBC Mkuu wa Moa akisakata twist na wageni toka Rwanda katika ufunguzi kyakailabwa.

Tumeelishwa vya kutosha na wengine tumejaliwa kuwa na uzoefu wa kutosha wa kuuza mkoa japo leo hii tunamtazamo mmoja ni miaka 50 ya uhuru jinsi tulivyodhubutu, kuweza na kusonga mbele kiuchumi, kiutamaduni, kijamii nk

Wajasiriamali hao ni nitawataja baadhi yao ni
1- KIROYERA TOURS- ikionyesha mambo ya utalii wa ndani na utamaduni wa mhaya zikiwemo senene, kahawa, masoma, ntura, na zana za kale za mhaya na kazi za mikono CD/DVD za saida Kalori na BK Sunday
2- AMIMZA- Kahawa
3. MAYAWA- Vanila
4. TANICA- kahawa

Wadau wenyewe ni Mkoa kwa maana ya RAS kagera, Nawapongeza kwani wametupa viongozi makini na ushirikiano mzuri sana wakiongozwa na Mr. Kisimba, Mr Ngirwa, Myuyu na IT Mr Samuel na ambao sijawataja majina pamoja na Halmashauri za Bukoba Vijijini, Karagwe, n.k Banda lake limependeza sana tupo kwa Mama Anna Mkapa building

Ukifika unaona wanakagera na ukarimu wa hali ya juu na nyuso za tabasamu za kutosha ukifika unakutana na banda la Mkoa likiwa limetengezwa kiasili kwa maana ya majani ya kukalia na mikeka uku pakiwa ba bronchure ( vipeperushi) na kinachofurahisha ni jinsi wanavyoonesha kwa kutumia power point DVD za Vita ya kagera, kagera profile ikiwa historia na utamaduni, utalii, watu wanavutiwa.

Leo tumepata wageni wengi siku ya ufunguzi kama mkuu wa Mkoa wa Iringa Mama Ishengoma, amependa kwao na kula senene toka Kiroyera tours, ameambatana na katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Mama Getrude Mpaka, na wengine wengi

Naushukuru uongozi wote wa mkoa wa kagera kwa kuwa karibu sana na kutoa ushirikiano mzuri na wadau toka sekta binasi

Tumefika salama na maadhimisho yameanza leo rasmi leo hii. Jana tulipata semina kidogo ya Customer care ( huduma kwa wateja) mtoa mada alikuwa kaiva na washiriki wamekubushwa jisi ya kumjali mteja ikiwa na aina ya wateja

Nakutumia picha waweza kuweka kwemye blog na kuwaomba wanabukoba walio Dar wafike sabasaba watuunge mkono maana tunautangaza mkoa pekee unaopakana na nchi tano za maziwa makuu ( uganda, Rwanda, Burundi, Congo na Kenya) na pia mkoa pekee ulipata madhara makubwa ya Vita vya Kagera na kuweza kusonga mbele kiuchumi, kiutamaduni, kielimu, kiafya, barabara na uongozi bora.

Ushauri wangu tusipende kulalamika tuwe na mtazamo chanya na kama unaona tatizo toa njia ya kutatua sio kulalamika. Tufanye kazi kwa pamoja

Kazi kwako kaka nitakuwa nakutumia matukio ya kila siku- kama kwao poa

Senene watapata fresh, kahawa safi, maji ya kabanga, mali juice, Rosela, banana wine, Utalii wa kitamaduni, CD za saida kalori na Bk sunday na Madawa ya asili na historia nzuri ya Mkoa wa Kagera

Karibuni tushirikiane ndo tutasonga mbele

Its me

William Oswald Rutta
Operations Manager
Kiroyera Tours
www.kiroyeratours.com
www.kagera.org
www.budap.org
http://www.facebook.com/pages/Kiroyera-Tours-and-Consulting/171058592931255
http://www.twitter.com/kiroyeratours
http://www.youtube.com/user/kiroyeratours

P.O. BOX 485
BUKOBA, KAGERA, TANZANIA

Tel: +255 28 2220203
Tel: +255-713-526649 or +255-784-568276
FAX: +255 28-2220009
Member of Tanzania Association of Tour Operator (TATO)
African Safari around Lake Victoria, Tour Operators, Travel Itinerary &
Booking Agents and Management Consultants

Cultural tours in Bukoba, Rubondo Island, Kigoma lake Tanganyika
Chimpanzees, Serengeti, Ngorongoro, Kilimanjaro,
Rafting on the Nile, Gorillas in Uganda and Zanzibar Island

Banda la Tanica
Kutoka kushoto ni mwakilishi wa Hamimza(kahawa),Mdau William Rutta wa Kiroyera Tours na wa mwisho ni mwakilishi wa Tanica.

Bukobawadau tunatoa pongezi kwa mashirika yote yanayo uwakilisha mkoa wetu pia tunatoa shukurani za kipekee kwa Kaka William Rutta kwa ushirikiano wako
Next Post Previous Post
Bukobawadau