Bukobawadau

MSANII ALPHA RWIRANGIRA KUMBE ANA ASILI YA KITANZANIA NA AMEWAHI KUISHI KAGERA!!!?

Alpha Rwirangira ni kijana mdogo anayetamba sana kwa sasa kutokana na sauti yake nzuri na kufanya vizuri katika mashindano ya TUSKER PROJECT yanayofanyika nchini Kenya kila mwaka,Historia yake hii hapa:

Alha Rwirangira alizaliwa nchini Tanzania Jijini Mwanza miaka 25 iliyopita Baba yake mzazi ni Mnyarwanda na mama yake ni Mtanzania mzaliwa wa Mwanza,Alpha ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watano wasichana wawili na wavulana watatu,alianzia elimu yake ya msingi katika shule ya Nyabohanse nchini Kenya mwaka 1993 kabla ya kuhamia shule ya msingi (Omukarilo Karagwe) Mkoani Kagera mpaka alipo hitimu elimu yake msingi yaani darasa la saba.

KUISHI BUKOBA
Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi Wilayani Karagwe,alikuja kuishi na wazazi wake waliokua wakiendeleza shughuli zao Mjini Bukoba na wakiishi maeneo ya Nyamkazi mpaka kufikia mwaka 2002, alipohamia Rwanda na wazazi wake,na kuendelea na Elimu ya Sekondari katika shule ya APRED NDERA mpaka kidato cha 6 akapata Diploma ya (MATHS AND PHYSICS)kwa elimu ya Rwanda,mnamo 2008.

Alpha alishiriki mashindano ya TUSKER PROJECT FAME 3 mwaka 2009 na akaibuka mshindi,kwa kuwapiga chini wasanii mbalimbali wa EA!!!hakuishia hapo kwani anaendelea kufanya vizuri katika sanaa na fani nyigine na hivi sasa anamiliki kampuni ya kutengeneza Viatu vya ngozi nchini Rwanda.

Mwaka 2011 Alpha ameshiriki tena mashindano ya TUSKER ALL STARS yaliyokuwa yanawakutanisha wasanii tofauti walio wahi kushiliki mashindao hayo ya TUSKER PROJECT FAME 1,2 na 3 na hapo pia akaibuka mshindi!!kwa sasa Alpha anaendelea a sanaa na amefanya kazi na wasanii wengi hapa EA kama A.Y amaye ni binamu yake wa damu,Ally Kiba wote wa Tanzania,Bebe cool na Bob Wine wote kutoka nchini Uganda na kwa sasa ameshatoa album yake ya kwanza inaitwa 1 AFRICAN!!imebeba nyimbo kumi,na anakaribia kutoa album yake ya pili!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau