Bukobawadau

Manchester United yaivutia kasi Man.City

Manchester United imezidi kuipa shinikizo Manchester City iliyo kwenye kilele cha Ligi kuu ya England kufuatia mkwaju wa Danny Welbeck dakika chache kabla ya mechi kumalizika. Mwanzoni mwa mechi hii United ilikua nyuma kwa pointi sita baada ya Manchester City kuirarua 

Tottenham hotspurs 3-2 kwenye uwanja wa Ettihad mapema siku ya jumapili.
Manchester United iliongoza kwa bao la Antonio Valencia dakika moja kabla ya kipenga cha mapumziko kuipa klabu yake bao 1-0. Bao hilo lilifutwa na la nahodha wa Arsenal katika kipindi cha pili na kuonekana kama liliowaamsha wachezaji wa Arsenal. Mabadiliko yaliyofanywa na pande hizi mbili hayakuonekana kubadili mchezo ingawa wadadisi wengi wanajiuliza sababu iliyomfanya Arsene Wenge kumuondoa mchezaji wake aliyeonyesha mchezo mzuri Alex Oxlade-Chamberlain. 

Licha ya juhudi na kuonyesha matumaini ya kuongezea mabao kwa Arsenal Manchester United ikitumia uzowefu wake na kuzingatia mpango wake waliokuja nao waliendelea kuizuia Arsenal isifurukute na kama ilivyo tabia yao ya kukamilisha tamaa yao dakika za mwisho,zikisalia dakika tisa kabla ya kumalizika kwa mechi Danny Welbeck akatikisa nyavu za Arsenal na kuipatia ushindi na pointi tatu. Arsenal 1 Manchester United 2. .
Next Post Previous Post
Bukobawadau