Bukobawadau

MDAU TUMUSIME BOCKO MJINI HAPA:Mjuwe mchezaji Mkongwe Maulid wa Buyekera.

Mc Baraka kushoto nikiwa na mdau kutoka Chicago Tumusime Bock ilimladhimu kutaka kunijua pia juu ya libeneke hili la Bukobawadau
Pichani ni Wachezaji wa Bukoba veteran.Picha hii imelenga kumuongelea Maulid Maulaa mzaliwa wa Buyekera kata ya Bakoba pichani niwa pili kutoka kulia mwenye Jezi Nyekundu ni kipa mzuri,maarufu na mwenye uzowefu wa kutosha mpaka hii leo kila siku yupo mchangani.

Maulid kacheza Fc Kombora enzi hizo,kacheza RTC Kagera ya Mshindo Madega na Kabaijo kama makocha...kabla ya kuelekea nchini Uganda na kujikita kusini kitongoji cha Nakaselo aliendelea kuchezea timu mbalimbali na kwa mafanikio makubwa.Kikubwa aliweza kurudi Bukoba na kuipandisha daraja timu ya Polisi Mkoa chini ya Jamal Rwambo na Seleman Kazembe kama watu wa soka.

Maulid nje ya kucheza timu kama Santos,Kayanga FC. Masaka Fc na Balimi ya akina Rama Kadomola au Mwamba Sele na kushiriki mashindano mbalimbali ya kimkoa ,kirafiki,na ya jimbo.
Bukobawadau tunasema huyu ndiye mchezaji aliyetumika sana kizazi hiki
Utaratibu wa kumpongeza kupitia Blog hii unaendelea kwa kushirikiana na wadau wenzangu Al Amin Abdul,Abdul Kapenter.Mdau Msese wa Bandarini,Uncle Jimmy,Uncle Shebby NSSF.Mdau Peter Mgisha,Mohammed Kassim na Kaka Mkuu hii yote ni kutekeleza maadhimio.

Salamu za mwaka mpya kutoka NY mtoto Azad H.Byabusha anawatakia wadau wote heri ya mwaka mpya 2012.
Next Post Previous Post
Bukobawadau