Bukobawadau

MWAKA 2012 UJANJA NI KUPUNGUZA MATUMIZI YASIYO NA LAZIMA;Harusi ya Mdau Joseph Mulokozi na Bi Leoncia Alimwambaza!!!

Bwana harusi Joseph Mulokozi kushoto na Bi Harusi Leoncia Alimwambaza na wapambe wao . Baada ya Ndoa takatifu hapa ni sherehe fupi iliofanyika nje ya Ukumbi wa Bukoba Club


Bukobawadau tunawapongeza maharusi hawa baada ya kufunga ndoa yao takatifu na kufatiwa na sherehe fupi ya watu wanne tu kwenye viwanja vya Bukoba Club.

Kuna haja gani vikao kumi vya maandalizi mpaka usiku wa manane hadi mkuu wa mkoa kalipigia sana kelele. Vikao vingine watu wanakaa mpaka kuumwa na Mbu.

 Michango mpaka mamilioni wakati elfu 20 tu inatosha na kwa Bukoba mjini sasa Kapu la mama (mjuburo),siku ya harusi yenyewe Burudani,mc,zawadi ya mama,Mjomba, Bibi,Babu, mshenga, Wanakamati,Vikundi vya kukopeshana vya kinamama hapo sasa wanakuja wanawake 20 wamebeba ndoo moja ya plastik inauzwa elfu 4000.

 Foleni ya Chakula ndefu kama foleni ya Sukari,Kufungua muziki saa 8 Maharusi wapo hoooi(chockest ile mbayaaa)yote ya nini?!!

 Bukobawadau tunawapongeza sana wadau hawa na huu ni mfano bora.
Next Post Previous Post
Bukobawadau