Bukobawadau

KAMPUNI YA KIROYERA TOURS YAUNGA MKONO JUHUDI ZA MKUU WA MKOA WA KAGERA; Mh.Masawe

Mdau Willy anatuonyesha parking ya mji mdogo wa Kigali-Rwanda 

Katika kuendeleza usafi wa mji wa Bukoba na wilaya zake zote. Manager wa Kampuni hiyo alifanya ziara ya wiki moja nchini Rwanda katika mji wa Kigali ili kupata mafunzo na kujionea siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi jinsi wanyarwanda wanavyohakikisha kasi ya usafi na mazingira inakuwa ya kweli.

Pamoja na kutemeba Kigali mara nyingi sikuwahi kufika siku ya usafi japo mji ni msafi kuliko miji yote unayoifahamu katika Africa mashariki na kati ikiwemo Bujumbura, Kampala, Nairobi, Dar es salaam, na Kinshasa pote tumetembelea Kigali ni namba moja. 

Siku hiyo hakuna matembezi aina yoyote wala biashara yeyote kufunguliwa isipokuwa hospatli na pharmacy tu. Hakuna gari kutemebea, wala piki piki, wala kituo cha mafuta wala baiskel wala mtembea kwa mguu, wala muuza magazeti, wala usafiri wa aina yeyote Ukiwa mgeni ndiyo unaweza kutembea na kufaidi wakati ukijifunza. Watanzania tuliobatika kuishi karibu na Rwanda wakazi wa kagera Kibali hutolewa bila kuchakachuliwa kwa mjonjwa na mtu mwenye emergency. najiuliza Watanzania tutafikia huko? Mkuu wa Kagera anatupa njia sasa

Kiroyera Tours inawakaribisha 
Watendaji wa serikali, 
Wafanya biashara wote,
Wenye Ngo za Mazingira 
Walimu na vyuo

Njooni tumuunge mkono Mkuu wa Mkoa wa kagera na tuwe watalii wa kiroyera Tours Twende tukatembee wakati tukijifunza na kuona mji wa kigali unavyokuwa kuliko miji yote ya Afrika mashariki na kati Kwa laki mbili tu unapewa usafiri kwenda na kurudi, kulala siku mbili na breakfast, visa ya kwenda Rwanda, kutemebelea vivutia vya utalii, kutembelea makumbusho ya mauwaji ambayo hatutapenda yarudie popote duniani na kuona mji ulivyo mzuri. Tutatembea na kwenda kwenye club za usiku za kigali kama KBC n,k 

Wasiliana na Willy Kiroyera 0784 56 82 76 Kiroyera Tours www.kiroyeratours.com www.kagera.org www.budap.org http://www.facebook.com/pages/-Tours-and-Consulting/171058592931255 http://www.twitter.com/kiroyeratours http://www.youtube.Kiroyeracom/user/kiroyeratours

P.O. BOX 485 BUKOBA, KAGERA, TANZANIA
Next Post Previous Post
Bukobawadau