Bukobawadau

UWANJA WA CCM KIRUMBA YANGA YATEPETA YACHAPWA 3-2 NA TOTO AFRICANS.

Kocha mkuu wa Toto ambae ni mchezaji wa zamani wa pamba na toto Africans Athuman Bilal akiwa ni mwenye furaha sana baada ya kuinyuka Yanga magoli 3-2

Mnazi wa timu ya simba mkoani mwanza Waziri Kabago akiwa na furaha sana baada ya filimbi ya mwisho,ni vigumu kujua furaha yake ni ushindi wa toto au ni kufungwa Yanga,je TOTO wakiwafunga simba atapenda pia?tafakari
<><><><>
<><>
Mdau erasmus George Rweyongeza aka Misifa akiwa uwanjani CCM kirumba na mameneja wake Hamimu na Raster

Camera yetu ilipomfikia Mdau Erasy alidai kuwa amegundua kuwa kazi zikiwa nyingi ni vyema kila kona ya Nchi ukawa na meneja wa kuratibu kazi zako.
Mdau kutoka Bukoba mwana serengeti bia nae alikuwepo uwanjani.
Basi la timu ya Toto lilitoka uwanjani kwa kusukumwa na mashabiki.
Wadau wa Mza wakiwa wameungana kuipa moyo timu yao,namuona Fulgence Novatus,waziri Kabago na Mh.diwani Mabura wa kata ya Mkolani,na aliyekuwa mgombea wa udiwani kata ya kirumba kwa tiketi ya CCM Mdau Jackson Robert Nyamtondo Jack (masamaki)
Namuona  OMGJames Mgaya (kushoto) , Noel Nyamubi na meneja wa Erasy Misifa bwana Hamimu

Next Post Previous Post
Bukobawadau