Bukobawadau

HIVI NDIVYO ILIVYOKUA KWA MDAU MUBELWA BANDIO -JANA KATIKA SIKU YA HABARI

 Mdau Mubelwa Bandio(kushoto) anayechukua masomo ya habari nchini Marekani na hivi punde tu atarejea Nyumbani kuonyesha alichonacho katika tasnia hii.

Baada ya kupata picha hii niliongea nae kutaka kujua ni nini kinachoendelea ili  nijuwe ubunifu wake kiutafiti na kwa faida ya wadau wengine na haya ndio maelezo yake;"Kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo, tunatakiwa kuandaa kipindi ambacho kitarushwa kwenye kituo cha chuo. Na kundi letu liliamua kujikita zaidi kwenye utamaduni wa kiChina.
 Tulimhoji Profesa toka China na kundi la muziki wa Opera la kiChina linalofanya shughuli zake hapa Marekani, taarifa mbalimbali kuhusu nchi ya China hapo nilikuwa nimemaliza mahojiano na mmoja wa vijana wenye asili ya China lakini wamezaliwa hapa Marekani kuona namna ambavyo wanakabiliana na mchanganyiko wa tamaduni mbili.
Huyu hapa pichani anazaliwa na Baba mwenye asili ya China na Mama Mmarekani."..alisema Bandio!!!
 
BUKOBAWADAU TUNAKUPONGEZA SANA KWA HATUA ULIOFIKIA  NA TUNAKUSUBIRIA NYUMBANI KAMA MZEE WA CHANGAMOTO  PIA TUJULISHE NAMNA GANI TUNAWEZA KUSIKILIZA VIPINDI VYAKO!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau