Bukobawadau

DK. STEVEN ULIMBOKA AJERUHIWA VIBAYA NA WATU WASIOJULIKANA.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Mama Dr. Kijo Bisimba akiwa na  Dk. Steven Ulimboka katikaa gari wakielekea MOI 
Dk.Steven Ulimboka pichani akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana baada ya kutekwa na kupigwa usiku wa kuamkia leo na  kuokotwa huko Mabwepande.

HII NI HABARI ILIYOCHUKUA KASI NCHI NZIMA NA KAMA KAWAIDA BUKOBAWADAU TUMEPITIA KURASA MBALIMBALI ILI KUPATA MAONI YA WADAU JUU YA TUKIO HILI;
  • Rahimu Bora uchungu wanajisikia madktari wenzake ndo sisi tunavyojisikia. ndugu zetu wanakufa

  • Andrew Peter Kato Kwa maelezo yako hapo juu bila shaka umefurahi sana alichofanyiwa Dk. Ulimboka
  • Jim Mteba Inasikitisha na kutisha,unyama gani huu!!!??
  • Edwin Mushema Mungu atamsaidia?
  •  
    Rahimu Bora hayo ni mawazo yako ; sisi tunauguliwa wazazi wetu wa matatizo ya vibofu, moyo,stroke
  • Elina Lutainulwa its too bad thou kushindana na mtu aliyeshika mpini na wewe umeshika makali ni mbaya sana
  • Andrew Peter Kato unauzunguka mbuyu tu Rahimu Bora, why dont you send your meseji straight! Kwani Ulimboka ndiye kawaletea wazazi wako matatizo ya vibofu, stroke na moyo? Hizo lawama itupie serikali yako
  • Gordon Chigudulu Wewe Rahimu una matatizo... Take a look at a bigger picture!
  • Rahimu Bora what is big pic. @Gordon ,@Andrew kato swala sio kuzunguka watu wanauchungu km uuguliwi shukuru Mungu.
  • Malkia Divina Mwafongo SUCH A PAINFUL THING.. NI UDHAIFU WA HALI YA JUU..
  • Andrew Peter Kato I feel very sorry for that level of myopic thinking and attitude my friend
     Zitto KabweNimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
    Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.
    Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.
    Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.
    Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’
    Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.
  • Arnold Dennis Kallape JAMANI HII NDIYO LIWALO NA LIWE!!!!!?
  • Beatrice Msacky Mungu amlinde na amsaidie apone Haraka.
  • Marie Kitunga Aisee tumefikia unyama wa aina hii sasa hivi? Shameless government of ours
  • Beatrice Msacky Halafu haya Mambo ya nayaonaga kwenye Movie tu. Duh live live . Hata Mungu Hapendi Jamani sio vizuri
  • Victor Deo Au ni Wagonjwa wenye hasira kali ndio wamemfanyia ili Madaktari warudi kazini....A
    Peter Matete Mc pole na kazi! Pia namtakia Dr Olimboka afya njema
     
  •   Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi amesema serikali itachunguza na kuwakamata waliohusika na kumteka na kumpiga Dr. Ulimboka
     
    Rahimu Bora Wazazi wangu walinifundisha ukiwa kwenye mgomo; Usikae mbele wala nyuma ; mpk leo sijui mantiki ya maneno yao
  • Osward Modest ‎. . . . . . . is this a solution? suala ambalo mtu hulitenda kama hatua ya mwisho hudhihirisha kwamba uwezo wake wa kufikria umeishia hapo. tunaelekea wapi?
  • Alex Lubida Pole sana ndugu Ulimboka, huu ni unyama mbaya sana
HII NI KATIKA KUPERUZI  KURASA MBALIMBALI

Next Post Previous Post
Bukobawadau