Bukobawadau

MISS LAKE ZONE INTER-COLLEGE 2011 KUFANYIKA BUKOBA TAREHE 23-6-2012

Malkia wa mipasho na mshindi wa tuzo za Tanzania Kili music Awards 2012 Khadija Kopa anategemewa kuwa kivuto kikubwa kwa kutoa burudani ya kipekee katika shindano la kumsaka mlimbwende wa MISS lAKE ZONE INTERCOLLEGES 2012 ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika mkoani Kagera katika mji wa Bukoba.
  Akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es salaam Mwandaaji wa shindano hilo Bw.Joseph Rwebangira amesema kuwa asilimia kubwa ya maandalizi yameshatimia,hata hivyo Rwebangira aliongezea kuwa mshereheshaji wa siku hiyo atakuwa mchekeshaji maarufu afrika mashariki na kati Mpoki wa the origina comedy.
   Miss Lake zone Intercolleges 2012 inayoandaliwa na kampuni ya Angles Real Entertainment ya jijini Dar es salaam chini ya Mkurugezi wake Joseph Rwebangira imejipanga vya kutosha kuleta mabadiliko ikiwa na lengo la kumfikisha mrembo wake katika ngazi ya fainali kitaifa.
   Shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa Linas Night Club uliopo Bukoba mjini siku ya jumamosi tarehe  23 juni ambapo mbali ya hayo kutakuwa na burudani za ngoma za asili na wasanii wa mkoa wa Kagera,pia kiingilio kitakuwa ni Tsh 10,000/= kawaida na V.I.P ni Tshs 15,000/=

BUKOBAWADAU BLOG NI WADHAMINI WAKUBWA WA ONYESHO HILI!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau