Bukobawadau

WADAU WA MAZINGIRA NA UTALII(KAGERA ENVIRONMENTAL CARE)KATIKA SHUGHULI ZAO

WAJUWE  KEC:Kagera Environmental Care(KEC)ni asasi isiyo ya kiserikali yenye makao yake makuu mjini Bukoba na shughuli zake kuu zikiwa ni uhifadhi wa mazingira na ushawishi kuhusu utalii endelevu katika mkoa Kagera.KEC imesajiliwa rasmi chini ya sheria Na.24 yamwaka 2002 ya asasi za kiserikali (NGOs)na kuanza shughuli zake rasmi July 2005.

 Malengoyao ikiwa ni kuongeza uelewa na hamasa kuhusu hifadhi ya mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali zeu,kutoa hamasa kwa wadau wa utalii kuhusu umuhimu wao kushiriki kikamilifu katika shughuli za kuhifadhi mazingira na huduma za kijamii.,kutoa elimu ya mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali na kuhamasisha umma kuhusu utalii wa kijani(green eco-tourism)kama shughuli mbadala ya kujiongezea kipato tofauti na zile zinazo changia uharifu wa mazingira.

Miradi mbalimbali iliyoanzishwa na KEC ni pamoja na huu wa upandaji wa miti katika fukwe za ziwa victoria.
 Mdau pichani ni Ndg Silvester Ndundulu ni mlinzi na mtunza mazingira.
Sehemu ya miti iliopandwa Mjini hapa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau