Bukobawadau

WASHIRIKI KATIKA SHINDANO LA KUMSAKA MISSS UTALII KAGERA 2012 WATEMBELEA BANDARI YA BUKOBA NA MELI YA MV.VICTORIA

Dinna Fashion kwa kushirikiana na Kiroyera Tours waandaji wa Miss Utalii Kagera 2012 waendeleza mikakati ya kuwajuza warembo mambo mbalimbali ususani ya ndani ya Mkoa wa Kagera
Pichani Kaka Mkuu akisalimiana na Warembo  hawa na kuwaambia karibu katika bandari ya Bukoba
Kaka Mkuu akitoa maelezo ya  awali mara tu baada ya kusalimiana na Warembo hawa, pembeni ni Bi Dinna , Mkurugenzi wa Dinna Fashion waandaaji wa Shindano la Miss U talii Kagera 2012 litakalofanyika mjini hapa  tarehe 14/7/2012 katika Ukumbi wa Linas Night Club.
Walimbwende wakisikiliza maelezo ya Kaka Mkuu kwa umakini  kabla ya kumkaribisha Afisa wa Bandari kwa maelezo zaidi
Afisa wa Bandari Mdau Ajuaye Kheri Msese akiwapa somo walimbwende katika kuwapa uelewa zaidi wa mambo mbalimbali.
 Mfanyabiashara maarufu mjini hapa Mama Stella katika picha ya pamoja na walimbwende hawa.
 Mwonekana wa Chumba safi cha daraja la kwanda ndani ya meli ya Mv. Victoria
 Washiriki wakipata maelezo kama sehemu ya huduma bora na kuwajali wateja , anaonekana Ndg Alex akitoa ufafanuzi zaidi juu ya vitanda safi na imara .
 Juu ya usafi sina swali?
Yoye juu ya yote ni pale walipokutana na Ndg John sehemu ya kupata vinywaji na chakula na akawapa maelezo ya kina.
Walimbwende hawa  wameweza kujua mengi juu ya bandari na Meli ya Mv Victoria, Meli kongwe ziwani victoria , yenye kuaminika inayotoa huduma safi ya usafiri wa abiria na mizigo kati ya Bukoba na Mwanza kupitia bandari ya Kemondo.
 Warembo wote hawa niwamkoa wa Kagera yote juu ya yote ni wewe mdau kufika kwa wingi tarehe 14/7/2012 ndani ya Linas Night Club ujionee kwa ukaribu watoto wa kibukoba walivyo babu kubwa,rangi rangi, guu guu tena la kihaya mdau usipime!!!!!!
 Hakika juhudi za Dada Dinna zinapaswa kuungwa mkono amekua mstari wa mbele kuinyanyua Kagera na na vijana wake kupitia urembo na mavazi.
Yeye makazi yake yapo jijini Dar es Salaam ila ni mdau anae kumbuka kwako,walimbende hawa wamemwaga sifa nyingi sana kwa Dada Dinna na Kampuni ya utalii ya ya Kiroyera na wenyeji wao kwa siku ya leo Bandari ya Bukoba.
 BUKOBAWADAU BLOGSPOT IS THE BEST…….!!!!

.
Next Post Previous Post
Bukobawadau