Bukobawadau

AJALI YA GARI LA OFISA WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA KATIKA ZIARA YA MHE. SAMWEL SITTA WAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI. JANA tarehe 29/08/2012 Katika  ziara Mheshimiwa Samwel Sitta Wazira wa Jumuiya ya Afrika Mashari Kutoka Wilaya ya Karagwe kuelekea Wilaya ya Kyerwa kulitokea ajali ya garia la Ofisa wa Ubalozi  wa Tanzania Nchini Uganda aliyekuja kuungana na Mhe. Sitta katika ukaguzi wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ajali hiyo ilitokea muda wa saa 5:15 asubuhi katika eneo la Lukole katika Kata ya Ihanda baada ya kuyumba na kuacha njia na kuangukia upande mmoja. Katika ajali hiyo hakuna mtu yeyote aliyeumia wote Ofisa wa Ubalozi na Dereva wake walitoka salama jambo ambalo halikuidhuru ziara ya Mhe. Sitta na kuendelea mpaka Wilayani Kyerwa Murongo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau