Bukobawadau

KITENDAWILI CHA UJENZI WA SOKO KUU MJINI BUKOBA CHATEGULIWA WADAU WATIA BARAKA ,MAENEO MBADALA YATAJWA!!!!!!

Sakata la ujenzi wa soko la kisasa mjini hapa leo limefikia  malidhiano kati ya Uongozi wa Manispaa na wadau wamiliki wa vyumba vya biashara ndani na nje ya soko kuu, Pichani mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Ndg Khamis Juma Kaputa akiongea na wadau walio hudhulia mkutano huo uliofanyika hii leo katika Uwanja wa Kaitaba.
Mdau Audax Matias akitoa vipaumbele vyake katika swala zima la ujenzi wa soko jipya ikiwa ni pamoja na kuutaka uongozi wa  manispaa kufanya uwakiki kwa wapangaji wa manispaa na wanao pangishwa
Mdau Aziz Abdulheri mfanya biashara wa Urembo mmiliki wa kibanda no.61 akitoa maoni yake
 Mdau Bi Zainab Maijani  mmiliki wa kibanda namba 9  akitoa ufafanuzi juu ya uwepo wa viongozi wa wafanya biashara waliopelekea swala hili lifike mahakamani  hivyo anawaasa wadau wachaguwe uongozi mpya kutokana na mkutano wa leo
Anaitwa Bi Gelaidina George mfanyabiashara wa ndizi aka (mpogole)
Wadau wakifuatilia maoni

Wafanyabiashara wakiwa katka hali ya  sintofahamu.
 Mh. Meya Anathory Aman
 Hotuba nzuri  ya Mh. Meya ikiwafurahisha wadau waliojitokeza
Baadhi ya wazee wanaomiliki vyumba eneo la sokoni
Sehemu ya wadau wakionyeshwa kufurahishwa na  maamuzi yalitolewa.
Ujio wa Mkuu wa Wilaya ya Bi Bukoba Mama Pangani
Sehemu ya wadau husika
Mkutano huu umefikia tamati kwa kuelezwa maeneo mbadala yatakayo tumika kama Soko ikiwa ni Jengo la CCM,sehemu ya uwanja wa shue ya Bukoba sekondari, Soko la Nyakanyasi na soko la Kashai .
Next Post Previous Post
Bukobawadau