Bukobawadau

WAISLAMU MKOA WA DODOMA WAMELAANI KITENDO CHA KIBAGUZI



NA Peter Mkwavila Dodoma.

WAISLAMU mkoa wa Dodoma wamelaani kitendo cha kibaguzi kilichofanywa
na mwalimu wa chuo kikuu cha St.John Tanzania kwa kuwalazimisha
wanafunzi wa dini ya kiislamukatika chuo kufanya mtihani siku ya
sikukuu ya Eid-al Fitri jambolililosababisha wanafunzi hao kukosa
fursa ya kuungana na waislamu wenzaokatika kuswali ibada ya Idd.

Akizungumzana waandishi wa habari,Shekh mkuu wa mkoa wa Dodoma Mustafa
Rajabu Shabanialisema kuwa kitendo kilichofanywa na chuo cha St.John
Tanzania si chakiungwana na kwamba kinaweza kuibua chokochoko za udini
jambo ambalo siutamaduni wa watanzania.

“Kitendohiki kwa kweli ni sawa na kuamsha chokochoko za kibaguzi
katika misingi yaudini,sisi wana Dodoma hali hii yatujaizoea hivyo ni
vema kamauongozi wa chuoutamchukulia hatua mwalimu aliyehusika na
kitendo hiki,mimi sitaki kuamini kamakweli yalikuwa ni maamuzi ya chuo
lakini imani yangu itakuwa sahihi kamamwalimu huyo atachukuliwa hatua
na sisi kupatiwa taarifa,”alisema Shekh wa mkoa

Aliongeza kuwaameamua kumuagiza katibu wake alifuatilie suala hili kwa
uongozi wa chuo nakwamba majibu yatayopatikana ndio yataonyesha kama
chuo hicho kimeamuakuchochea ubaguzi katika misingi ya udini ama
ulikuwa ni udhaifu wa mwalimuhusika.

“Suala hilisio kwamba limeleta fedheha kwa wanafunzi ambao ni waumini
wa dini ya kiislamupekee bali hata kwa wakristo maana sisi tulizoea
kuishi kama jamaa moja,mambokama haya ndio yanaweza kusambaratisha
ujamaa wetu na sisi wana Dodoma hatupotayari kuona mtu au taasisi
yoyote ikitusambaratisha katika misingi ya udini,ndiomaana nasema
mwalimu huyo achukuliwe hatua kali.”Shekhe Mustafa Rajabu alisemana
kuongeza,

“Hili sijambo jema wala zuri,serikali imeheshimu siku hii na kutenga
kuwa ya mampuzikokatika mawizara na taasisi zote,kitendo hiki mimi
nimekilaani,huyo mwalimuachukuliwe hatua ambayo mwalimu mwingine
watajifunza,hili si jamo zurilimeniuzi,nimelilaani sana,nasisitiza
hatua zichukuliwe ili walimu wengine iweni wa
St.John,UDOM,Hombolo,Mirembe na hata sekondari weheshimu na
kujifunza,”alisisitiza.

Kwa upandewake Makamu mkuu wa chuo hicho Prof Gabriel Mwaluko alisema
kuwa hana taarifajuu ya tukio kama hilo na aliahidi kulifuatilia na
kulipatia ufumbuzi.

“Sinataarifa hiyo,ngoja niifuatilie kwa sababu mkuu wa chuo (Town
Campus) nimuislamu,hebu ngoja niifuatilie”alisema Prof.Mwaluko.

Naye mwalimuanayetuhumiwa kutoa mtihani siku ya Idd aliyetajwa kwa
jina la Allen Mtetemela alikana kuhusika katika kitendo hicho na
kusema kuwa yeye si mwalimu husika wasomo.

“Nanikakupatia namba yangu,nitajie jina la mwanafunzi huyo kwa
mfano,mimi bwanasiwafundishi somo hilo hivyo siwezi kuwapatia mtihani
wa somo ambalo sifundishi”alijibu Mtetemela.

Hata hivyowanafunzi walidai kuwa ni kweli Mtetemela sio mwalimu wa
somo hilo la sherialakini aliwalazimisha kuja kufanya mtihani huo
ambao haupo hata kwenye karendaya chuo kwa madai kuwa mwalimu ambaye
amekuwa akiwafundisha hutunga mtihanirahisi mno.

Agosti 19,2012,siku ya jumapili ambayo pia ndio ilikuwa sikukuu ya
Idd,chuo kikuu cha St.John Tanzania kiliendesha mtihani kwa wanafunzi
wanaosoma stashahada ya sheria jamboa ambalo lililalamikiwa na
wanafunzi husika hasa wa dini ya kiislamu na walilazimika kufikisha
malalamiko yao kwa shekhe wa mkoa kwa madai kuwa wamenyimwa fursa kwa
maksudi ya kushiriki katika ibada ya idd.

Chuo kikuucha St.John Tanzania kinamilikiwa na kanisa la Anglikana
Tanzania,hata hivyo kimekuwa kikidahili wanafunzi mbalimbali pasipo
kutumia vigezo vya dini au madhehebu.

MWISHO………………………………………………………
Next Post Previous Post
Bukobawadau