Bukobawadau

CHRISTINA SHUSHO KUPAMBA UZINDUZI WA ALBUM YA YESU NI MWEMA YA KAPOTIVE.

Ndugu wadau tumsifu Yesu Kristu. Tar.23/12/2012 kwa mapenzi ya Mungu, kutakuwa na uzinduzi wa album ya Kapotive Star Singer Vol: 1 ya Yesu ni Mwema, na utambulisho wa album yao Vol: 5 ya "NAKUSHUKURU MUNGU". Kwa wale ambao watkuja Bukoba kipindi hicho, tafadhali pata ticket yako mapema. Katika uzinduzi huo utasindikizwa na Padre mchezaji (The dancing Priest) Fr. Anthony Musaala, na mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Dada Christina Shusho, kwaya za RC, ELCT na SDA za hapa Bukoba zitachuana. hama kwa hakika itakuwa siku ya kipekee Bukoba. Tafadhali fikisha habari hizi kwa rafiki yako ambae unafahamu  yupo mjini hapa au atakuja Bukoba kipindi hicho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau