Bukobawadau

KAMATI YA BUNGE YA SHERIA NDOGO YAWASILI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE MKOANI KAGERA


 Wajumbe wa  Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo Wakiongozwa na Mwenyekiti Wao  Mhe. Sylvester Mabumba Wakiwa Katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mh. Fabian Massawe
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akiwapa Maelezo ya Utangulizi na Halisi ya Mkoa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo

Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Sylvester Mabumba pamoja na wajumbe wake wapo mkoani hapa kupitia, kuona na kuchambua sheria ndogo katika Halmashauri za Wilaya za mkoa wa Kagera ili sheria hizo kupitishwa kwa ajili ya kutekelezwa.
Aidha kamati hiyo ipo hapa mkoani kuona changamoto zilizopo katika kutekeleza sheria ndogo za Halmashauri za Wilaya au ni wapi sheria hizo zinakwamishwa, na kotopitishwa kwa wakati ili ziweze kutekelezwa kwa wakati .
Akitoa ufafanuzi wa kutekeleza sheria ndogo katika mkoa wa Kagera Mkuu wa Mkoa mbele ya Kamati hiyo katika ofisi yake, alisema pamoja na upungufu wa watumishi katika Halmashauri za Wilaya lakini sheria ndogo mkoa wa Kagera zimeweza kurekebishwa na kuenenda na mazingira ya kukusanya mapato.
Pia mkoa wa Kagera umeweza kutunga sheria ndogo ya kuunda mfuko wa elimu na baadhi ya Halmashauri za Wilaya tayari zimeunda mifuko hiyo. Sheria ndogo ya kuhakikisha wananchi wanatekeleza usafi katika maeneo yao, aidha sheria hizo zinaibuliwa kutoka kwa wananchi wenyewe na wananchi wana mwamko wa kuitikia kutunga sheria hizo ndogo.
Pamoja na mafanikio hayo lakini Mkuu wa Mkoa alibainisha pia changamoto katika kutunga sheria ndogo, kuwa ni upungufu wa Wanasheria katika Halmashauri za Wilaya, sheria ndogo kuchelewa kuidhinishwa ili zitekelezwe kwa wakati, baadhi ya sheria ndogo kupitwa na wakati, pia baadhi ya sheria ndogo kuwabana wananchi hivyo kutokea sheria hizo kuchukiwa na jamii.
Kamati ya  Bunge ya sheria ndogo itafanya majumuisho yake mkoani Kagera kesho tarehe 19/10/2012 mara baada ya kumaliza kazi zake.
 Mheshimiwa Aden Lage akiondoka Ofisini Kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa  tabasamu pana.
Next Post Previous Post
Bukobawadau