Bukobawadau

MCHAKATO WA KUSAKA VIPAJI VYA FILAMU 26 BORA WAINGIA KAMBINI HII LEO CHINI YA YA ZACHWA INVESTMENT

Hawa ndio wasanii Mkoani Kagera waliofanikiwa kuingia 26 bora katika usahili wa kusaka vipaji vya filamu wakiwa katika viwanja vya Bukoba Club tayari tayari kabisa kuingia kambini.
Kwa mbali anaonekana Chief Judge Bi Regina Mganyizi akiwapa wasanii maneno ya mwisho mwisho kabla ya kuingia kambini.
Mkurugenzi wa ZACHWA  INVESTMENTNdg Mganyizi akitoa neno pia kwa mbaali anaonekana mdau Rahim akifatilia kwa umakini mkubwa zoezi hili.
Hizi ni swagga tu za wasanii katika utayari wa kuelekea kambini.
Sehemu ya wasanii katika picha ya pamoja muda mchache kabla ya kuelekea kambini.
Wakufunzi vinara wa filamu mjini hapa kutoka kushoto ni ndg Hamad na ndg Sudy katika picha ya pamoja na mmoja wa wasanii anayefanya vyema  ndg Odda Man Obed
Kundi la wasanii wa kiume waliong'aa  sana  katika hatua za awali na tarifa ni kwamba  toka tumeanza kukujuza habari hii tayari wasanii wote wapo kambini na huduma wanayopata ni ya hali ya juu kama chama la Madrid.
Anaonekana Kaka Mkuu akiwa na Mkurugenzi wa ZACHWA INVESTMENT ,Mdau Jamal pembeni DJ, Sley wa 88.5 Kasibante FM Radio na  Chief Judge Bi Regina mwenye mkoba.
Uratibu wa shughuli hii ukiendelea na mikakati ya kimawazo mawazo nje ya viwanja vya Gymkhana.
Fainali ya usahili huu itafanyika  siku ya Ijumaa 5/10/2012  ndani ya Linas Night Club ambapo waasanii nyota wa Bongo movie  pichani watakuwepo ili kuakikisha Mkoa unapata wasanii bora

BUKOBAWADAU BLOG TUNATOA PONGEZI KWA KAMPUNI YA ZACHWA INVESTMENT KWA KAZI HII KUBWA YA KUWASAIDIA VIJANA WETU HAPA KAGERA,TUNAWAOMBA WAKAZI WA MKOA WA KAGERA KUJITOKEZA KWA WINGI SIKU YA IJUMAA KUWAONA WASANII WETU WAKIWA SAMBAMBA KABISA NA WASANII WAKUBWA KAMA JB , UWOYA NA NDAUKA NYOTE MNAKARIBISHWA.!!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau