WATU WATATU WAKAMATWA NA BUNDUKI NA RISASI 96 SERENGETI
na pascal michael buyaga
serengeti
Watu watatu
wakazi wa kijiji cha motukeri katika wilaya ya Serengeti mkoani mara,akiwemo
raia wa nchi ya Kenya wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani mara kwa tuhuma
za kukamatwa na bunduki aina ya smg Fn na risasi 96 kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo kamishina msaidizi Absalom mwakyoma amethibitisha kukamatwa kwa
watu hao ambao amewataja kuwa ni sabasaba makuru kambarage (31),Timothy Bernad
omoke (20) raia wa Kenya na pius mayengo sengeka( 43) wote wakiwa wakazi wa
kijiji hicho kilicho kata ya nata wilayani Serengeti.
Kamanda mwakyoma amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa
octoba 23 majira ya saa mbili na nusu
usiku mwaka huu katika kitongoji cha mageriga nyumbani kwa mtuhumiwa wa kwanza
sabasaba wakimiliki silaha hiyo ya kivita
kinyume cha sheria
Amesema kuwa Maafisa wa polisi wakishirikiana na maafisa wa
shirika la hifadhi Taifa (TANAPA)siku ya tukio baada ya kupata taarifa kutoka
kwa raia wema walifanya msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na
vipande 10 vya nyama kavu ya pori ,mikia sita ya nyumbu na mayai mawili na
maganda mawili ya mayai ya mbuni kinyume cha sheria ambapo thamani ya nyara
hizo hajafahamika.
“ Polisi wakiwa katika msako mkali wa kuwasaka wahutumiwa hao
walifika kijijini hapo majira ya saa mbili na nusu usiku ndipo waliwakuta ndani
ya nyumba hiyo walimokuwa wakihifadhi nyara hizo na kisha kufanikiwa
kuwakamata”alisema kamanda mwakyoma.
Inadaiwa kuwa bunduni hiyo imekuwa ikitumika kuulia wanyama
pori na wakati mweingine vitendo vya uharifu sehemu mbalimbali hapa nchini na
kuhatarisha usalama na maisha ya
wananchi pamoja na mali zao.
Kamanda alisema kuwa
upelelezi utakapo kamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua
zaidi za kisheria na ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi kufichua na
kuwataja waharifu.