Bukobawadau

ZOEZI LA KUUFANYA MKOA WA KAGERA KUWA KIJANI LAZINDULIWA RASMI RWAMISHENYE BUKOBA

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Akipanda Mti Katika Mji wa Bukoba Katika Uzinduzi wa Zoezi la Kupanda na Kutunza Miti 12,500,000 Mkoani Kagera
 Anaonekana MdauHuyu Stelle Andrew Mtumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pia naye Akipanda Mti katika Zoezi hilo Pia AKiwakilisha Akina Mama wa Mkoa wa Kagera.
 Jeshi la Polisi Pamoja na Kudumisha Ulinzi wa Raia na Mali Zake Lakini Nalo Lilishiriki Katika Kupanda Miti Kama Kamanda Huyu Unavyomuona Hapa.
Watoto nao Hawakuachwa Nyuma na Wanafunzwa Kukua na Tabia ya Kupanda Miti na Kuitunza pia ili Nao Iwatunze Kama Wazee Wanavyofanya.



Mkuu wa Mkoa wa Kagera azindua rasmi zoezi la kupanda miti katika mkoa wa Kagera na uzinduzi huo ulifanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba eneo la Rwamishenye  tarehe 25/10/2012, zoezi hilo la kupanda miti lilianzia Bukoba katika sehemu mbalimbali za mji ambapo wananchi na watumishi
wa serikali katika idara mbalimbali walihusika kupanda miti na jumla ya miti 400 ilipandwa siku hiyo.

Mkoa wa Kagera umejipangia kupanda na kuitunza jumla ya miti 12,500,000  kwa mwaka 2012/2013 na katika zoezi hilo kila Halmashauri ya wilaya  inatakiwa kupanda na kuitunza jumla ya miti 1,500,000. Miti inayoendelea kupandwa mkoani Kagera ni pamoja na miti ya matunda, mbao pia na vivuli.
Upandaji wa miti katika mkoa wa Kagera ni endelevu kwani wananchi wamehamasika katika upandaji na utunzaji wa miti. Lakini Mhe. Massawe anahamasisha zaidi wananchi kupanda miti ya matunda ili kutunza mazingira, lakini pia wananchi kujipatia matunda kwa ajili ya kuboresha afya zao na biasharaa  maana miti ya mbao tu ndiyo imekuwa ikipewa kipaumbele na wananchi katika maeneo yao.
Akitoa ufafanunuzi Afisa misitu wa mkoa Bw. Jafari Omari zoezi hilo kuzinduliwa mwezi Octoba alisema, ni kutokana na kipindi hicho kuwa na mvua za wastani za vuli na miti ikipandwa wakati huo ni rahisi kuota kuliko wakati wa kipindi cha masika ambapo miti mingi huoza au kupata mstuko kwasababbu baada ya masika hufuata majira ya kiangazi.
Vile vile Mhe. Massawe  amewashukuru sana wananchi wa mkoa wa  Kagera kwa kuwa waelewa pale wanapoelezwa kuhusu maendeleo ya mkoa  wao. “Nawashukuru sana wananchi wa Kagera kwa kudumisha usafi katika mkoa wetu na kuitikia zoezi la kupanda miti, usafi umetuletea sifa kubwa sana ndani na nje ya nchi yetu kutokana na uelewa wenu ( Uinshomile) na nasistiza tuendelee kutunza mazingira yetu . Alishukuru Mhe. Massawe.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa alitoa zawadi za Sikuu Kuu ya EID-ELL-HAJ iliyofanyika siku ya Ijuumaa kwa vituo vinne, viwili vinavyowatunza watoto yatima Uyacho Hamgembe na Nusuru Yatima Kashai vilivyoko katika Manispaa ya Bukoba.
Vituo vingine ni kituo cha Mtakatifu Nicholaus Kemondo kinachowatunza watoto wenye mahitaji maalum, pia kituo cha Kuwatunza Wazee Kiliima vilivyoko  katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba. Vituo hivyo vilipatiwa mchele kilo 50, mafuta ya uto lita tano na mbuzi mmoja kila kituo.
Mhe. Massawe baada ya kutoa zawadi hizo alitumia nafasi hiyo kutoa tahadhari kupita vyombo vya habari kuhusu wananchi wa mkoa wa Kagera kudumisha amani na kuachana na uchochezi baina ya dini moja na nyingine ili wananchi waendelee kuishi kwa amani utulivu na upendo miongoni mwao.
Next Post Previous Post
Bukobawadau