Bukobawadau

KIBAKA WA SENENE ANASWA NA NGUO ZILIZOIBIWA KWA MAJIRANI

Camera yetu katika pitapita maeneo ya Uswahilini Bilele inakutana na tukio hili,ambapo kijana mmoja akiwa ameambulia kichapo kwa kile kinacho semekana kuwa ni kibaka.

 Mashuhuda wa tukio hili wametunyetisha kwamba Jamaa huyu ni mkazi wa maeneo hayo na hivi karibuni alikimbia na chungu cha senene  ndipo sakata likaanza chumba kwa chumba, shuka hadi shuka ili kutafuta  ni nani mwizi  hivyo wakaweza kubaini baadhi ya nguo zilizoibiwa kwa mmoja wa majirani kitendo kilichopelekea wananzengwo hao Vijana wa Mayunga  kuona inatosha  kwao wakawa wamejiridhisha na kuanza kumtembezea kichapo kama inavyo onekana pichani

HAYO NDIYO  MAMBO YA USWAZ!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau