HIVI NI VITUKO USWAHILINI
'Chankomele' na 'kuiringisa' ndio utamu wa ngumi za mtaani.
Ni ugomvi unaomhusisha kijana Mashavu kushoto na Baba Hafith ambaye ni shuhuda tu wakati mwenzake akiinama kuokota simu hiyo nokia 1280 maarufu kama nokia ya tochi yenye thamani ya shilingi elfu 45 za kitanzania.
Piga nikupige baada ya wadau kushadadia kwamba atakayeshinda katika ugomvi ndiye mwenye haki ya kuchukua simu hiyo ,ni baada ya wao kushindwa kuelewana.Sakata hili limeendelea mitaa ya Manyema hotel .
Ugomvi ukiendelea kutafuta mmiliki halali.
'Deka haka ti kabana'!!Ni neno la kihaya lililo mtoka baba hafith baada ya kulemewa na kichapo,Pichani anaonekana akikimbia huku mdau akimpoza kwa kummwagia maji, akiongea Bukobaadau Baba hafithamesema; Haikuwa halali ingawa alijaribu ukauzu na kupambana ili kuona kama atapata mkate wa watoto nyumbani kwani angeweza kuiuza iwapo angefanikiwa!