Bukobawadau

KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI CHA KRFA

Wajumbe wa kamati ya utendaji wa Chama cha soka mkoa wa Kagera KRFA katika picha ya pamoja, wa tatu kutoka kushoto ni Mdau Jamal Malinzi mwenyekiti wa chama cha soka mkoa na kwa tiketi hiyo  anawania uongozi wa juu kabisa TFF kama Rais wa shirikisho hilo.
Kaka Didas Zimbihile katika sala ya kuombea kikao na Agenda zake.
Refa mstaafu Refa wa  kimaitafa mwenye Beji ya FIFA nae alikuwepo Mr Baijuka wengi tunamuelewa,hakika soka Kagera itasimama 

Pamoja na mambo mengine kamati imeomba watu wajitokeze kwa wingi kuipa kuipa nguvu Timu yao ya kagera kwa kufika uwanjani na kuishangilia maana duru la pili ni gumu kila timu inatoa macho kuhakikisha inapata pointi 3.
BUKOBAWADAU BLOG tunamuombea Mdau Jamal Malinzi aweze kufanikiwa katika harakati zake za kugombea uongezi wa juu kabisa wa TFF huku tukiwa na imani kuwa yeye ni mtu wa mpira wa miguu kwa muda mrefu pia kupata kwake ndio mafanikio kwetu maana tutajivunia Mwenyekiti wetu wa Mkoa ndiye Rais wa mpira wa Miguu wa Taifa, tunamtanguliza mungu huku tukijuwa kuwa mpambano ni mkali sana
Next Post Previous Post
Bukobawadau