Bukobawadau

MDAU ANAHOJI;Nani mwenye haki ya kupanga uzazi????

Ndg Wadau,

Limedondoshwa dawatini jana mchana...........Jamaa ameoa takribani miaka minne sasa. Mungu ni mwema kwa ndoa yake wana mtoto mmoja na maisha yanasonga japo milima na mabonde hayakwepeki. Gumu lililojiri ni hili, Jamaa kutokana na mpangilio wa maisha na uhalisia wa maisha ya Mtanzania anaona kuongeza mtoto mwingine si vyema kwa sasa. Mama yeye anataka mtoto mwingine, biashara asubuhi..... Jamaa kavuta hendibreki hataki na ametoa angalizo kwamba ikitokea mama amekubali mimba iingie, ole wake.

Hili lamsumbua mama na baba pia kila mmoja kwa mtazamo wake kama narration ilivyotanabaisha.............. .............

Mshauri wa Mahusiano (HATA WEWE WAWEZA KUWA)..............Shauri la kufanyika hapa!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau