Bukobawadau

BREAKING NEWS;Jengo lenye Ghorofa 16 limeanguka katikati ya Jijji la Dsm mtaa wa Indira Ghandi, na inasemekana huenda zaidi ya watu 60 wamefukiwa na Jengo hilo lililokuwa linaendelea kujengwa.

 Ni tukio la kuuzunisha na kusikitisha,Jengo la ghorofa 16 laporomoka katikati ya viunga vya Jiji la Dar
 Ni tukio la kuuzunisha na kusikitisha,Jengo la ghorofa 16 laporomoka katikati ya viunga vya Jiji la Dar





 Rais Kiwete akiwa mitaa ya Hindira  Ghandi jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri
Mpaka sasa watu wawili inasemekana wamepoteza maisha na watu 17 wameokolewa ,zoezi la uokoaji waliofukiwa kwenye kifusi linaendelea kwa juhudi, na uchunguzi wa nani anajenga na nani msimamizi unaendelea,endelea kufuatilia bukobawadau kupata kinacho.
Rais Jakaya Kikwete mchana huu ametembelea eneo lilipoanguka jengo la ghorofa 16 katika makutano ya Barabara ya Zanaki na Indra Ghandi na kuhimiza juhudi za uokoaji ziongozwe ili kuokoa maisha ya watu wanasadikiwa kuwa wapata 60 waliofukikwa ndani ya Kifusi.Tayari askari wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT) na lile la Wananchi(JWTZ) wapatao 500 wako eneo la tukio katika juhudi za uokoaji.
Juhudu za kuokoa watu waliofukiwa zinaendelea muda huu ingawa vifaa ni duni.
Next Post Previous Post
Bukobawadau