HUKUMU YA MSANII KAJALA IMETOLEWA
Habari njema kwa mashabiki wa muigizaji Kajala Masanja ambaye leo hukumu yake imesomwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa
kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na
mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.
Taarifa kutoka mahakamani zinadai kuwa wasanii wa bongomovie wanachanga
fedha hizo ili wazilipe na tayari inasemekana Wema Sepetu amezitoa
fedha hizo zote kutoka mfukoni mwake.
Mrembo huyo na mumewe Faraja Chambo
walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu ambayo ni pamoja na kula njama
ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa kwa kuhamisha umiliki
wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.
Shtaka la pili ni ni kwamba Aprili 14
mwaka 2010 waliamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kinyume na
kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya
mwaka 2007. Shitaka la tatu ni la kutakatisha fedha ambalo walilitenda
Aprili 14 mwaka 2010 huku wakijua ni kinyume cha sheria.
Hakika Wema anajua kujijengea Kesho yake.
Hakika Wema anajua kujijengea Kesho yake.