Masheikh wa Uamsho wabadilishiwa mashtaka
Zanzibar: Washtakiwa wa kesi inayowakabili viongozi wa Jumuiya
ya Uamsho na Mihadhara ya Kidini (Jumiki) Zanzibar, wamesomewa mashtaka
mapya katika Mahakama Kuu.
Mwendesha Mashtaka, Ramadhan Nassib aliyasoma mashtaka hayo mapya yanayowakabili mbele ya Jaji Fatma Hamid Mahamoud.
Nassib alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na madai
ya kuharibu mali, uchochezi, ushawishi na kuham asisha fujo na kula
njama ya kufanya kosa.