MTANZANIA JUMATANO MACHI 27;Sakata la Lwakatare: Mbowe na Dr. Slaa kuhojiwa
TUKIO la kukamatwa
na kufikishwa Mahakamani kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare, kwa tuhuma za
ugaidi, huenda likasababisha kukamatwa au kuitwa kuhojiwa kwa
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, MTANZANIA Jumatano
linaripoti.
Mbali na Mbowe, kwa mujibu wa habari zilizolifikia gazeti hili, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa huenda naye akajumuishwa katika mahojiano hayo.
Habari zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa, Mbowe au Slaa watahojiwa baada ya polisi kukamilisha upelelezi wake na mtuhumiwa mwingine aliyeshitakiwa pamoja na Lwakatare, ambaye pia ni kada wa chama hicho, Ludovick Rwezaura.
Chanzo chetu cha habari, kililidokeza gazeti hili kuwa, hatua ya akina Mbowe kukamatwa au kuhojiwa inakuja kutokana na viongozi hao kuhusishwa na tuhuma kama zile zinazowakabili Lwakatare na Ludovick.
Inaelezwa kuwa baada ya kukamatwa kwa Lwakatare pamoja na Ludovick na kufanyiwa mahojiano ya muda mrefu, walibaini kuwa viongozi hao, wanahusika katika tuhuma hizo za kupanga mipango ya kigaidi.
Taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa na vyombo ambavyo vinapeleleza tukio zima la akina Lwakatare zinaeleza kuwa uamuzi hasa wa kumkamata Mbowe umefikiwa baada ya kutajwa kuwezesha kimkakati na kifedha katika mipango hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mbowe kama Mwenyekiti wa chama hicho wanamuelezea kwamba sauti yake ni kubwa katika kuhakikisha mipango hiyo inafikiwa, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha fedha kwa ajili ya idara inayoongozwa na Lwakatare, ambayo ni mahususi kwa kufanikisha ulinzi na usalama wa chama.
Gazeti hili lilipomtafuta Mwenyekiti wa chama hicho, Mbowe, kupitia simu yake ya kiganjani ili athibitishe kama tayari wamekwishapokea wito wa kutakiwa kuhojiwa, simu yake haikupokelewa na hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakujibu.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, alipotafutwa na MTANZANIA Jumatano kupitia simu yake ya kiganjani ili kuthibitisha hayo, alisema wao hawajaitwa kuhojiwa na wala hajui kama wataitwa.
Pia alieleza kuwa jukumu la kuthibitisha kama chama chao ni cha ugaidi ni la mahakama.
“Hatujaitwa kuhojiwa na polisi na wala sijui kama tutaitwa kuhojiwa na jukumu la kuthibitisha ugaidi ni la mahakama, kama mtu au watu wanasema sisi ni magaidi mahakama ndiyo itasema na kutoa uthibitisho.
“Hivi kama mtu akisema wewe ni mchawi inamaanisha kweli wewe ni mchawi, si mpaka athibitishe, kwenye siasa kuna mengi, tunasemwa mengi kama chama.... Tumeshaambiwa tumemuua Chacha Wangwe, tumeshaambiwa sisi wadini lakini tupo tu,” alisema Dk. Slaa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alisema lipo chini ya timu ya watu 12 iliyoundwa na kwamba hawezi kuzungumza lolote.
“Timu ile ya watu 12 iliyoundwa kwa ajili ya uchunguzi wa sakata la Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, ndiyo inahusika katika matukio yote ya ugaidi, ikiwemo kutekwa kwa watu mbalimbali na kutishiwa waandishi wa habari, hivyo watakuja na majibu yao kuhusiana na kile watakachobaini,” alisema Kamanda Kova.
Hatua ya kutaka kuwakamata au kutaka kuwaita akina Mbowe inakuja wakati ambapo kwa muda mrefu wapinzani wao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamekuwa wakiwashutumu Chadema kutekeleza mipango ya kigaidi kwa siri.
Miongoni mwa tuhuma ambazo CCM walizielekeza dhidi ya Chadema ni pamoja na ile ya kudaiwa kuingiza makomandoo kutoka nchini Afghanistan, Israel, katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, madai ambayo pia yalidaiwa kutekelezwa na Chadema katika chaguzi ndogo za Tarime na Arumeru Mashariki, ambapo inadaiwa kuwa vijana hao walikwenda huko kufanya fujo.
Hata hivyo, Chadema kimekuwa kikikanusha madai hayo, kikisema kuwa ni njama za CCM kutaka kukidhoofisha chama hicho.
SOURCE: MTANZANIA